.

Mjasiriamali Tawala Mawazo Yako



Meshack Maganga (Go Big):

Habari za Asubuhi, WAJASIRIAMALI wenzangu ? Awali ya Yote, Ninapenda kumshukuru Kwa Asubuhi hii. Ni Asubuhi Njema kabisa Na Kwa Mjasiriamali tunasema ni Fursa.kubwa kabisa kuliko kuliko zote ulizopata kukutana nazo...

Iwapo Jana ulikuwa unatafuta mtaji, una unafasi kubwa sana Leo ya kupata mtaji Huo...Leo, una unafasi ya kukutana Na Mshauri uliyekuwa unamtafuta siku nyingi, una nafasi ya kwenda popote utakapo...Na Tena una nafasi ya kusoma kitabu cha Mafanikio ulichokuwa una kisikia Kwa Muda mrefu.

Takari Yetu Ya Leo, itahusu  "Mjasiriamali Tawala Mawazo  Yako " .. Kwenye Jamii zetu, watu wengi Wana ndoto kubwa sana, lakini wamekuwa wakirudishwa nyuma Na mawazo dhaifu Kutoka "nje " ninaposema nje Nina maana nje ya wewe, nje ya Malengo Yako...Wengi tumekuwa tukipanga mawazo Na ndoto za kufika mbali, lakini badala yake tumekuwa tukirudishwa nyuma Na watu wa karibu Yetu. Watu hao tunawajua...

Tunakula nao, tuna kunywa nao na pengine tuna wanunulia Vocha Na wanatumia Vocha hizo, kutukatisha tamaa. Tunafahamu kwamba Mwanadamu aliuumbwa akiwa kamili lakini baadae akageuka Na kuwa anavyotaka...

Kuna binadamu walioumbwa vizuri lakini baadae " Wamejiumba Na kuwa " Mawakala " wa kukatisha wenzao tamaa, kazi yao ni kuzodao...mnafahamu kuzodoa? Nilipokuwa kidato cha kwanza wenzetu wa kidato cha pili walikuwa wanatuzodoa kwamba hatujui kuongea Lugha ya mkoloni... Nimetolea mfano.

Mjasiriamali na mkulima wakati umefika ambao unatakiwa kuchekecha mambo...wakati umefika wa kumsahau " shosti " uliyesoma nae chuo, unaeruka nae viwanja, unaechati nae kwenye mitandao, unaekula nae chips, umefika wakati wa kusimama wewe kama wewe.

Maana bila kufanya hivyo utajikuta Muda umeenda, huna chochote zaidi ya kuwa mpiga debe wa Malengo ya wenzako...utajikuta unaendelea kupanga Na kupanga, mikakati isiyokuwa  mwonekano...
Sikilizeni niwaambie. Kuna wanajamii ambao Hata uwaeleze Nini, Hata kama ungenena Kwa Lugha, wataendelea kutukatisha tamaa, kuna binadamu ambao hawapaswi kusikia ndoto zako, wanatakiwa waone...kwakuwa ndoto huanzia kwenye Umbo lisilo onekana, yani Wazo, ni Bora liendelee kukaa Huko kichwani kwako, kuliko kumweleza " Dream killer " maana atakukatisha tamaa... Umefika wakati wa kuangalia ni Yupi role model wako, ambae ukimweleza ndoto Yako atakusaidia kuifikia.

Fahamu kwamba, kuna mipango ambayo huna budi kuifanya bila kuitangaza. Itakapo onekana kwenye Umbo la nje hao hao waliokuzodoa lazima watakusifu...😀💪 wataanza kusema " Tulijua lazima ufanikiwe, watasema Yule ni balaa...wakatisha Tamaa ndio hivyo hivyo, Hata mbinguni walikuwepo, wakatimuliwa...


Unataka Ku- Go Big ? Andaa Malengo Yako kimya kimya,usiropoke Kwa wajuaji , Hao wanaojiita " University Thinker " wakisikia unafuga Simbilisi, unafuga Sungura, unalima bamia, unauza nguo, unafuga bata, ama unataka kununua kiwanja msata, ama unataka kupanda Embe, utasikia, " Huyo GPA yake ni below standard, huyo alisoma chuo cha kata...nk. Watakuzodoa...hao hao " University Thinker wanapokuwa kwenye majengo ya chuo, wanajiona wapo kwenye ulimwengu mwingine Na kusahau mtaani kwao...Subiri watoke chuo sasa, Maisha yanavyowapiga, utawahurumia wanavyo tembeza bahasha zenye GPA... Utawahurumia wanavyo saga sori ofisi Kwa ofisi....Na wewe Mfuga Simbilisi Na mlima bamia Na Mfuga kuku unapeta maana Tayari utakuwa Na kibunda mfukoni...

Mjasiriamali Tawala Mawazo Yako...Ni wakati wa kumsahau shosti wako wa chuo Na kukazania Malengo Yako...Na uchaguzi unabakia mikononi mwako...Go Big or Go Home and watch TV, japo nimesikia wanaangalia Tv nao wanachangamoto, katikati ya movie umeme unakata...

Mjasiriamali Tawala Mawazo Yako...



Posted via Blogaway...GO Big g or Go Home


Previous
Next Post »