Na: Meshack MAGANGA, Go Big Movement.
Habari za Asubuhi, WAJASIRIAMALI wenzangu? Awali ya Yote, ninapenda Kutumia Nafasi Hii, kumshukuru Kwa kutulinda wiki hii Yote.
Pia, ninawapenda Kuwashukurua Wana - Go Big wote, Kwa Michango ya Mawazo mbali mbali ya kuhamasishana mliyoitoa wiki nzima hii inayoisha Muda Mfupi Ujao.
Tunakaribia kuimaliza wiki hii. Na kama ilivyo kawaida, sina budi kuwaletea Tafakari ya kufunga wiki.
Tafakari Yetu Ya Kufunga wiki inasema " Ukikumbuka ulipotoka huwezi Kudharau Fursa "
Kila Mwanadamu Duniani Kwa umri alionao sasa anafahamu vizuri historia yake ya Maisha. Anafahamu alipokuwa Mdogo alishi Maisha Gani, wazazi wake walitumia mbinu Gani kumlea Na kumkuza Mpaka akafikia pale alipo. Wengi kama siyo wote wanakumbuka Hali yao ya Maisha ilivyokuwa enzi hizo wakiwa watoto Wadogo. Na si ajabu Kila mmoja wetu bado yupo kwenye Mchakato wa Maisha wa kufikia kwenye Ndoto zake. Na Ama Kwa hakika Kila mmoja wetu Na Jambo linaloibeba picha ya Maisha yake.
Iwapo ungetolewa Muda Wa Kila mmoja wetu kuelezea historia ya Maisha yake , vingetokea vicheko ama vilio.
Tunakumbuka enzi hizo unarudi Kutoka shule ukifika Nyumbani unakuta jiko limenuna Na chakula hakuna. Ama upo shule Muda Wa pumziko umefika wenzako wanachagua wanunue Nini Na wewe midomo imekaukiana.
Siku Moja nilikuwa Na rafiki Yangu Wa karibu sana Hapa Go Big, alinisimulia historia yake Kwa kifupi sana alivyokuwa akilazimika Kutoka kwao Na kwenda sehemu Nyingine kufanya vibarua vya kubeba mizigo sokoni...Niliumia lakini nilijifunza kwamba hakuna Mwanadamu anayezaliwa kisha apitie raha milele bila changamoto. Ni wakati Huo nilikumbuka mabafu ya Hostel ya shule niliyosoma , nilikumbuka vile vipande vya sabuni , mabaki Ya sabuni niliyotumia enzi hizo.
Tafakari Yetu Ya Kufunga wiki inasema " Ukikumbuka ulipotoka huwezi Kudharau Fursa "
Kutokana Na mabadiliko mbali mbali ya Kijamii, kwenye Taifa letu, Fursa nyingi nimekuwa wazi sana Na kutokana Na maendeleo ya teknolojia Tumepata bahati ya kuletewe fursa viganjani mwetu.
Mimi kama Mimi Nina ushuhuda mkubwa sana, kuna Fursa nilikuwa sijapata kuzisikia Wala kuziona, ama niliziona Na kisha nika zishaua. Nitolee mfano wa parachichi, ukweli nimeziiona tangu nikiwa mtoto mdogo lakini kujua kwamba ekari Moja itaweza kunipatia Milioni 30 ni kitu nimekijua mwaka Jana.
Nilijifunza Limao, bamia, Nyanya chungu, Viazi , mihogo, Ufugaji kuku, nimesikia Mengi Kwa wenzangu nikasafiri sana, nikajifunza BIOGAS, Sungura, Simbilisi, Uuzaji wa Senene, Na juzi Hapa nikasikia Mende Hawa Mende Ni Bonge la dili. Wiki haijaisha nikasikia Ekari Moja Ya Passion ni zaidi Ya milioni 14 hasa ikimkuta asiye jishaua, juzi tena nikasikia Uyoga , Uyoga Uyoga, si kwamba Haya mambo ni Mageni hapana, kuna tatizo la kuona Kwa jicho la Ndani.
Nimekaa nikakumbuka vipande vya sabuni kwenye mabafu ya shuleni kwangu viliponiokoa siku zile EMS imechelewa ... Nikakumbuka Na hizi Fursa nikamshukuru Mungu.Kwa kuniunganisha na watoa mada zote humu ndani.
Kisha nilikumbuka nilipojisingizia kwamba, nimefunga, ulipofika Muda Wa Kula kumbe sina hela ya chakula. Na nikazikumbuka hizi Fursa za kumwaga. Nilikumbuka enzi zile kijiji kwetu kulikuwa Na duka kubwa la Na nilijionea wanakijiji wenzangu walivyokuwa wakidaiwa pesa Na mwenye duka ... Nikajitafakari sana.
Tafakari Yetu Ya Kufunga wiki inasema Ukikumbuka ulipotoka huwezi Kudharau Fursa...
Na ukimbuka Maisha Yako Ya mwaka Jana ama mwezi uliopita huwezi Kudharau Fursa, ukimbuka Maisha ya Kila siku tunayoishi unaweza Kutoa machozi.
Ukiona Maisha wanayoishi wanadamu waliofanikiwa huwezi kuchezea Fursa.
Kumbuka Tu ulipotoka, kumbuka Maisha ya kazini kwako, kumbuka kauli za bosi wako, kumbuka maneno ya mtoto wa bosi wako, kumbuka foleni za kwenye Taasisi za Kutoa mikopo, jiangalie mfukoni,
Nk. Utajikuta huna sababu kusingizia Na huwezi kujikuta una chelewa kufanya maamuzi.
Ukiona huna cha kukumbuka kwenye Maisha uliyopita, utakuwa ni Mwanadamu wa kipekee sana.
Uchaguzi ni wetu, Na kupanga ni kwetu, ukikutana Na waliofanikiwa iwe ndani ya kundi ama nje waulize walianzaje...Moja Kwa Moja watakumbuka Walipotoka ... Watakupa Hamasa...Uchaguzi unabakia mikononi mwetu, kukumbuka tulipotoka ama Kuendelea kusubiri mujiza wa kujipatia kipato na kutafuta waombeaji wakati mujiza upo kwenye kuzalisha Uyoga ama kufuga Mende Na kuwauzia wa China...
Fursa za Mafanikio Zinaanzia Kwa Mungu Na ni Mali ya Mungu. Chanzo cha umaskini kwenye Jamii Yetu kinachangiwa Na mambo Mengi, kuna wanaozijua Fursa hawataki kwajulisha wengine wanataka wenzao waendelee kuwa omba omba , wanataka wenzao waendelee kufulia Na kuangushwa Na vifafa vya kiuchumi. Na kuna waliozisikia Fursa wanaendelea kujishaua...
Wanaziona Fursa za bamia kitu gani,? Niliwahi kusema kwamba, " ukimuona Sungura ukasema umemwona Tembo , siku ukimuona Tembo utasema umeona kitu gani ?
.... Unaambiwa kwamba, ukila ugali Na mchina finyanga Tonge...
Na Tafakari Yetu Ya Kufunga wiki inasema Ukikumbuka ulipotoka huwezi Kudharau Fursa...
Wenu katika Fursa ya Passion. Meshack Maganga Go Big Movement...
Ninawatakia Jumamosi Njema yenye Mafanikio makubwa sana...
Sign up here with your email