.

Kinachoitatiza Dunia Kwa Sasa Ni Hiki Hapa



                         
Na: Meshack Maganga-Iringa

Kinachoitatiza Dunia kwa sasa ni hiki hapa:- Vijana wadogo wake kwa waume wanaohitimu vyuo mbalimbali wapo bize kusaka ajira, na wale ambao bado wapo shuleni na vyuoni na wao wana ndoto za kupata ajira (idadi yao ni kubwa sana). 

Na baadhi ya waliopo kwenye ajira wamechoshwa na ajira zao,wanafokewa kama watoto, wanakosa muda wa kufanya mambo yao, na wengine wanalalamikia mishara midogo. Mbaya zaidi waliopo kwenye ajira wake kwa waume, wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea hawapo tayari kuachia ajira zao. Unajua ni kwanini hawataka kuachia ajira zao?...Bado
wanajiandaa, na wengine hawajapata mitaji miaka nenda rudi. 

Ili kuondokana na tatizo la kutopata ajira (utakapo kuwa 'university thinker') na wale wazee wazima kuogopa kupoteza ajira zao, Vijana wa kike na wa kiume waanze kujifunza ujasiriamali kwa vitendo. Wewe Baba na wewe Mama wahamasishe watoto wako wajifunze kuwekeza wakiwa wadogo. Udongo uwahi ungali mbichi na samaki mkunje angali mbichi. 

Mwalimu wangu wa ujasiriamali na uwekezaji, Robert Kiyosaki alipata kusema kwamba 'Children do not know what ‘HOT’ means until they touch the stove ' Na wewe Mwalimu wa chuo ama shuleni wahamasishe wanafunzi wako wasitegemee ajira peke yake. (Na utakapo kuwa unawahamasisha wanafunzi wako ukumbuke kujihamasisha, Maana kuna idadi kubwa sana ya walimu wa ngazi zote wanao wafundisha wanafunzi ujasiriamali wakati wao wenyewe hata mabanda ya chips hawana, unafundisha nini sasa? unamfundisha mwanafunzi ufugaji wa ng'ombe Marekani, wakati wewe mwenyewe hata mbuzi huna, mwanafunzi atapata wapi hamasa? ). 

Na wewe Mwanasiasa acha kuwadanganya Vijana waliopo masomoni kwamba ukiingia madarakani utazalisha ajira za kumwaga (hahahaha, we mwenyewe umeajiriwa tena kwa muda na upo biz kuilinda hiyo ajira yako, hizo za kumwaga utazitoa wapi? think outside the box ) 

Na wewe mwanafunzi unapokuwa chuo ama shuleni, usibabaishwe na majina ya makampuni,mabenki,ama mashirika, wengi wetu tunapokuwa chuo tukisikia jina la kampuni kubwa,akili zetu zinawaza mishahara, ukishaajiriwa hapo unaanza kuuza muda wako, kumbuka hata wewe unaweza kuanzisha kampuni kubwa na ukaajiri watu. (I believe you are born with the responsibility and the obligation to make a positive impact) Uchumi wa dunia utayumba kabisa iwapo kila mtu atakuwa na ndoto ya kuajiriwa. There's Greatness in all of us.

Kwakua hatusomi na kujifunza na kuendelea kuwa na mawazo  na utamaduni wa Old stone age ama niite industrial age  tumezalisha imani na mitazamo mingi iliyo hasi kuhusu fedha na maisha kwa ujumla.  
Niliwahi kusoma makala moja ya Albert Sanga alisema kwamba, Kiukweli nchi hii imekuwa ikizalisha wasomi bandia kutokana na misukumo hasi. Wengi wanasoma fani ambazo sio za miito wala karama (talents) zao kwa sababu ya ama matarajio ya upatikanaji wa ajira ama upatikanaji wa mikopo. Ndio maana  watu wanayumbishwa kila siku, kwa sababu aliyetakiwa kuwa mfanyabiashara unamkuta kwenye udaktari, aliyepewa kipaji cha ualimu unamkuta benki na hayumkini tuna rundo la walimu katika mifumo yetu ya elimu ambao walitakiwa kuwa wanajeshi! (yale yale ya mwalimu kuripotiwa kucharaza viboko kwa kutumia waya!)

Fikra hizi za kusomesha watoto ama kusoma ili kuajiriwa ndizo zilizojaa katika fahamu za watanzania wengi. Kwa bahati mbaya sana, kutokana na mabadiliko ya mifumo ya kisiasa na mabadiliko ya uchumi wa dunia; matumaini ya kila anayehitimu masomo yake kuajiriwa yanazidi kuyeyuka siku hadi siku. Hapa nchini Tanzania hadi sasa, kuna nafasi chache sana za ajira ikilinganishwa na idadi ya wasomi inayotapishwa na rundo la vyuo vikuu na vile vya kati.

Ukiacha hilo la ajira kuwa chache, bado kuna changamoto kwa wale wanaobahatika kuajiriwa. Changamoto hii ni kutotosheleza kwa mishahara (na marupurupu) inayotolewa ikilinganishwa na hali ya maisha pamoja na malengo anayokuwa nayo mwajiriwa. Suluhisho ni ujasiramali huku tukiendelea na ajira zetu.
Mawasiliano:  email: meshackmaganga@gmail.com
Previous
Next Post »