Na: Albert Sanga, Iringa.
Mtu
anaponiambia kuwa huyu mtu ni msomi ama hiki kitu kimefanyika kisomi huwa
sitishiki wala kubabaika. Huwa natenganisha kati ya mtu kumiliki vyeti na mtu
kuwa na akili. Ukibahatika kuwa navyo vyote viwili basi una bahati lakini
wasomi wengi wanaishia kuwa na vyeti pekee; akili eidha hawana
ama huamua
kutozitumia.
Kuna
wasomi nilikutana nao 2012 pale Ilula wakaniambia wamefanya utafiti wa kilimo
cha nyanya na wamegundua kuwa biashara hiyo haina faida hata tone kwa namna
wakulima wanavyolima pale Ilula.
Kwanza nikashangaa, nikawaeleza, "mnasema
hakuna faida, mbona hizi nyumba na maendeleo yote Ilula ni matokeo ya nyanya,
kivipi hazina faida?" Wakanitolea magraph yao meeeengi, wakanipa sijui
nini nini sample za waliowahoji; yote wakitaka kunidhihirishia kuwa
walichonieleza kipo kisomi!
Mi nikawaambia labda mngeniambia wakulima
wanapata faida pungufu ya inayotakiwa lakini kusema kilimo hiki hakina faida
kabisa, nakataa! Nikaachana nao maana niliona wamenizengua tu. Msimu uliofuata
nikafanya biashara ile ya nyanya nikapata faida kubwa sana tofauti na
walichosema.
Hawa
wasomi kwenye biashara waonage hivi hivi, wana vimambo vyao vya kiutafiti
ambavyo ukisema uvizingatie vinaweza kugeuka miluzi ya kukupoteza ~SmartMind~
Sign up here with your email