.

Kuna Vitu Unavifanya Bila Kutumia Pesa...!

 Kuna vitu unavifanya bila kutumia pesa nyingi, mfano hizo mbegu za Parachichi nimepewa bure labda nauli ya daladala kutoka nyumbani shilingi mia 4 na kurudi mia 4. Hizo mbegu nitazipeleka shambani, kila mti wa Parachichi utaniletea pesa miaka michache ijayo. Zaidi ya hapo, miche itakayo zidi nitaiuza, kwa wakulima wenzangu watakao hitaji. Mche wa kawaida wa Parachichi huuzwa shilingi mia saba hadi elfu moja kwa Iringa. 

Lakini Nikizifanyia " Bading" Nitauza kwa shilingi elfu 3. Mtaalamu wa kufanya hiyo kazi yupo Ndugu Nicolaus Kulanga . Hii ni pesa na ni ajira kamili kwangu. Kumbuka nimeokota sokoni. Miparachichi ikifanyiwa Bading huanza kutoa matunda baada ya miaka mitatu hadi miaka minne. I wish I could tell you that the rest is history. 

Tanzania is a great country; the harder you work, the luckier you get. Na kama alivyo niambia Mkulima mwenzangu Hadija Jabiry (Mama B' Ministry)kwa msisitizo kwamba soma Yoshua 1: 9 ' Je si Mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na Moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike'... Na uchaguzi unabakia mikononi mwangu, Kuwa hodari na Moyo wa ushujaa ama kufadhaika. The cost of continuing to not get this knowledge is up to you. Nobody else. Go big or go home and watch Tv.
Previous
Next Post »