Na: MROPE wa MROPE
NDANI YA KILA MTU UNAYEMFAHAMU KUNA MTU MWINGINE USIYEMFAHAMU:
Kila
binadamu ana utu wa nje na utu wa ndani. Utu wa nje unaweza kuwa imara
kuliko utu wa ndani na utu wa ndani unaweza kuwa imara kuliko utu wa
nje.
Vyovyote iwavyo hatima ya maisha ya mtu huamuriwa
na
utu wa ndani. Huko ndiko mtu hufanya tafakari na kuchukua maamuzi ya
mwisho. Maana yake ni kuwa utu wa ndani ukiwa mlegevu hata maamuzi ya
mtu yatakuwa malegevu na matokeo atakayopata mtu huyo ni malegevu pia.
Kuna
wengine unaweza kuona ni jitu lenye afya njema na nguvu nyingi lakini
utu wake wa ndani ukawa dhaifu sana na hapo ndipo utasikia, "huyu mambo
yake hayaendani kabisa na jinsi alivyo".
Kuna mwingine
ana afya njema na ni pandikizi la mtu na utu wa ndani ni imara basi watu
watamsifu kwa kusema, "vile unavyomuona na ndivyo alivyo mpaka
'rohoni'".
Wengine wana miili midogo wanafanya mambo
makubwa, wengine umri mkubwa wanafanya mambo ya umri mdogo kabisa, kwa
hiyo ni wazi kila binadamu ana mtu wa pili ndanimwe ambaye anaathiri
fikra, matamshi, na matendo na hatimaye matokeo ya maisha yake. Katika
hali halisi ni nadra sana utu wa nje kuwa bora kama utu wa ndani ni wa
ovyo ovyo. Wengine utu wa ndani ni ovyo lakini kwa nje utu wake ni bora,
huyo si bora bali anapretend (kujishaua).
Kwa hiyo
jukumu la mtu kufanikiwa lazima lianze kujengwa kwa mtu wa ndani yako.
Ukiwa imara ndani hata kama nje watakudharau wala hutatishika. Huwezi
kusimamia maamuzi mazito ambayo jamii inayaona kinyume na ukabaki imara
kuendea malengo yako kama utu wa ndani ni legelege.
Malengo
yote ya mafanikio kwanza yanapata upinzani katika ulimwengu wa roho
toka kwa shetani na wajumbe wake maana mafanikio yako yanakuondoa katika
uwezekano mkubwa wa kunasa katka mitego yake mingi anayoitumia kupitia
umaskini.
Kuna vibaka, majambazi, makahaba, machokoraa,
ndoa zinazobomoka kupitia umaskini na kwa namna hiyo shetani ana
maslahi na umaskini na Mungu hajatuwekea fungu la kushindwa wala
umaskini ili kutuepusha na hayo.
Umaskini sio mpango wa
Mungu. Kwa hiyo mafanikio yako yanapngwa na shetani na kisha binadamu
wasiokutakia mema na ndiposa unapaswa kuwa imara katika utu wa ndani ili
usimame imara kuelekea maamuzi yako na kama haupo imara ndani utapga
mbwembwe na mayowe bila kufanikiwa.
Nini kifanyike? 1.
Jiimarishe katika imani ya kushinda 2. Jifunze kufikiri, kutamka na
kutenda katika kushinda 3. Fanya mafanikio unayoyatarajia kuwa sehemu ya
ukombozi wa wale wanaoteswa na kukosa mafanikio kama yale utakayoyapata
wewe. Imarisha utu wa ndani kisha uyaendee mafanikio yako. Che Mrope Wa
Mrope, Mbeba Maono (fb page), 0766656626/0715366010/0787641417
Sign up here with your email