.

Mafanikio Ni Kuondokana na Utumwa

MROPE Wa MROPE

Mafanikio sio kitu cha kawaida kama wengi wanavyofikiri na kuchukulia kirahisi. Mafanikio ni kuondokana na utumwa, mafanikio humpa mtu uhuru na uhuru humpa mtu furaha na furaha humfanya mtu kutenda mambo katika usahihi na hivyo kuchochea mafanikio maradufu.

Yumkini umepata kujiuliza kwanini wanaotenda haki mafanikio yao yanachelewa tofauti na wasiotenda haki, jibu ni jepesi kwamba mafanikio ya mtu asiyetenda haki hayana faida kwa jamii wala hayaleti mabadiliko chanya kwa jamii yake.

Pesa ya jambazi hununulia  silaha za kufanyia maangamizi lakini pesa za mwenye haki husaidia mayatima, hujenga nyumba za ibada na mengine yenye faida kwa jamii na kuipa jamii muelekeo chanya. Wasiotenda haki hufanikiwa haraka ili uharibifu uzidi kuongezeka hapa duniani.

Wanaotenda haki mafanikio yao huchelewa si kwa kuwa Mungu hapendi wafanikiwe ila wao wamesahau kama mafanikio yao yanakumbana na vikwazo vya yule anayewafanikisha waovu ili huyu anayetenda haki aende katika njia ile isiyo haki katika kutafuta mafanikio.

Mafanikio ni mafanikio tu haijalishi mtu amepata kwa njia gani lakini swali la kujiuliza ni, "mafanikio hayo yameleta furaha?" kama mafanikio hayajaleta furaha basi ni kujichosha tu maana juhudi zetu ni kupata furaha na sio kuitokomeza furaha. Kuwa kwenye jumba la kifahari huku mikono inanuka damu ni majuto na huzuni moyoni.

Kwa kuwa furaha ndio chemchem ya mafanikio yote basi uadui wa kwanza wa muovu ni kukuwekea vikwazo usifikie mafanikio kwa kukunyima furaha na kukujaza hofu.

Hakuna awezaye kutenda jambo na kufanikiwa kama amejaa hofu na mashaka na hayo ni matokeo ya kupoteza furaha.

Basi kwa maarifa haya unapaswa kufahamu kuwa njia mojawapo ya kuondoa hofu ni kufurahi hata kama huna sababu ya kufurahi, wewe furahi ili kufukuza hofu na uoga.

Umewahi kumuona mtu mwenye tabasamu muda wote amejawa na uoga? Mimi sijawahi kumuona. Kwa hiyo unaweza kushndwa kabisa kwenda kufanya mambo ya msingi kama huna furaha na umekaukiwa na amani moyoni. Amka ufurahi na utapata nguvu ya kutenda. Tukutane baadaye kidogo

Previous
Next Post »