.

Jinsi Ya Kuongeza Kipato Kwa Kanuni Rahisi.

Na: Paul Masatu.

Watu wengi wanajiuliza ni namna gani wanaweza kuongeza kipato chao? Labda unaweza kuona mazingira hayakuruhusu kabisa, ukipiga picha unaona hamna namna ya jinsi pato lako litaongezeka, hujui uanzie wapi! Kuna njia na mbinu nyingi ambazo zinafundishwa na nakutia moyo uzifuatilie zote kwa ukamilifu ili uweze kuongeza pato lako.

Lakini kama hujui kabisa wapi kwa kuanzia, leo naomba nikupe kanuni very simple ambayo ukiiweka kwenye vitendo, pato lako litaongezeka, ni simple but it is not easy, ubahitaji determination na bidii ili uweze kuona matokeo kwenye kipato chako.

Kanuni hiyo imejengwa kwenye hii simple formula

   Money= Energy

Nina maana gani ninaposema " Energy"? Naomba uanze kuyafuatilia maisha yako ya kila siku, hapa ninamaanisha yale mambo unayo yafanya mara kwa mara, kila siku, unaweza kuitumia hii wiki inayofuata kuanza kufanya utafiti huu, utagundua hii wiki nzima kuna ratiba yako, au mambo unayo yafanya ambayo yako fixed, yaani the whole week, kila siku, utakuwa ukiyafanya kwa kujirudia rudia( Routine), yaani inakuwa sehemu ya maisha yako, siku haiishi bila ya kufanya hayo mambo, wala hutumii nguvu kufanya hayo mbambo.

Sasa kwasababu ya kuyafanya mara kwa mara kila siku, kila wiki, kila mwezi na kila mwaka, yametengeneza mfumo fulani wa wewe unavyo itumia siku yako, wiki yako na mwaka wako, sasa huo mfumo umefungwa kwenye kitu tunaita " energy level" hiyo energy level ndiyo inakuwezesha uendelee kufanya hivyo hivyo( routine) kila siku, kila wiki na hatimaye kila mwezi na usipoangalia kila mwaka.

Hiyo energy level, iliyofungwa kwenye matendo yako unayo yafanya mara kwa mara, kwa kujirudia rudia, ndiyo inakupa pia level mbali mbali za maisha, ikiwa ni pamoja na level ya kipato (income level), kwahiyo pato lako la sasa ni matokeo ya hiyo energy level inayo operate kwenye maisha yako sasa hivi, ambayo imefungwa kwenye matendo yako ambayo ni routine.

      Money= Energy

Sasa unabadilishaje level yako ya kipato( income level)??

Unaanza kwa kubadilisha your level of energy, your energy level iki change na kipato chako kitabadilika, sasa swali linakuja how do you change your energy level? Unabadilishaje hiyo energy level??

Very simple, lakini its not easy kama nilivyo kwambia. Kwenye hiyo routine yako( hayo mambo ambayo unayafanya kila siku kila wiki kila mwezi kwa kujirudia rudia) chagua angalau moja( ukiweza kuchukua mawili matatu itakuwa vizuri zaidi) halafu badilisha jinsi unavyo Fanya( hiyo ndiyo maana nasema ni simple) lakini its not easy kwasababu utatakiwa hilo jambo moja au mawili uliloamua kulifanya kwa tofauti, itabidi uendelee kulifanya kwa tofauti hivyo hivyo mpaka linajenga mfumo wa energy na utakuwa unalifanya bila shida, yaani linakuwa sehemu ya tabia, kwa ku replace jambo jipya kwenye mfumo wako wa routine, utakuwa umebadilisha kabisa level ya energy yako kwasababu inabidi ipatikane new level ya energy ili iweze ku accommodate new routine, na energy level vikibadilika tu, kwa mujibu wa hii formula money=energy  na kipato chako kitabadilika kinaweza kuwa high( kikubwa) au low( kidogo) inategemea aina gani ya routine umeichagua.

Sasa mimi nikushauri two new routine, ambazo ukizijenga katiba mfumo wako wa maisha ya kila siku, your energy level itapanda( high) na utasababisha kipato chako kiongezeke.

1. Muda wa kuamka

Ule muda wako wa kuamka rudisha nyuma kwa lisaa limoja na amka lisaa limoja kabla, kama unakawaida ya kuamka saa kumi na mbili rudi nyuma amka saa kumi na moja, endelea kufanya hivyo mpaka iwe sehemu ya maisha yako, yaani iwe tabia yako, you will change your energy level.

2.  Soma kitabu/ vitabu

Kwenye routine yako iwe ya siku au wiki au mwezi, introduce new routine ya kusoma kitabu, nakwambia ukweli your energy level will change, na kuongezeka na itasababisha kipato chako kuongezeka, unaweza ukachagua jambo lolote lile, kama kuwahi kazini, kuanza kufanya saving, kuongeza idadi ya simu unazopiga kwa Mteja, kurudi shule na kuongeza elimu n.k na your energy level will change na kipato chako kitabadilika.

~Paul Masatu

Previous
Next Post »