.

Ni Mapenzi Ya Mungu Ufanikiwe Kiuchumi

Na: Paul Masatu
1. Ni mapenzi ya Mungu ufanikiwe kiuchumi.
- Ni mapenzi ya Mungu, uongezeke kifedha,
-N i mapenzi ya Mungu mali zako ziongezeke.
Moja kati ya maeneo katika maisha ambayo unatakiwa ukue na nguongezeka ni eneo la kiuchumi
* Unahitaji fedha na mali kwa ajili ya maisha yako binafsi
* Unahitaji fedha na mali kwa ajili ya kuujenga ufalme wa Mungu duniani
* Unahitaji fedha na mali kuwasaidia watu wengine, wahitaji na jamii inayo kuzunguka kwa ujumla.
Kwahiyo una kila sababu ya kufanikiwa kiuchumi, usipo fanikiwa kiuchumi, unakosa uwezo wa kuhudumia na kukosa kutoa mchango wako kwenye eneo moja wapo au yote niliyo orodhesha hapo juu.
Kuna baadhi ya mafundisho potofu yanayo husisha, maisha ya kupungukiwa fedha au mali, maisha ya umaskini na utakatifu, yaani wanajaribu kutenganisha ongezeko la mali na kuukosa ufalme wa Mungu, wanajaribu kujenga uhusiano wa ukata na kumtafuta Mungu, yaani kwa kadili mtu anavyo kuwa na dhiki ndiyo kiwango chake cha maombi, kuhudhuria ibadani na kumtafuta Mungu kwa ujumla kinavyo ongezeka.
No huu ni uongo mtupu, ni mawazo ya adui yaliyo pandikizwa kwenye akili za watu, ili kuwafanya watu kuendelea kuwa masikini zaidi, kuwafanya watu kuishi kwenye vifungo vya dhiki na mapungufu makubwa ya fedha.
Kwenye level ya nchi kuna falsafa inayo iliyo jengwa kwenye mawazo ya watu, ya kuhusisha umaskini na uadilifu, kiasi ambacho mtumishi wa umma au kiongozi, akimaliza uongozi au utumishi wake hana kitu, hata kibanda cha kukaa hana, tunampongeza na kumuona mfano bora wa uadilifu na uzalendo.
Na hii dhana imekuwa na negative effect kwenye jamii kwamba hauwezi kuwa tajiri, au hauwezi kufanikiwa kifedha na kimali, huku ukiwa muadilifu, tumeaminishwa ni lazima kwa namna moja au nyingine ufanye mambo ambayo ni kinyume cha sheria, kama ubadhirifu wa mali ya umma, wizi na ulaji rushwa ndiyo unaweza kufanikiwa kifedha, dhana ya wingi wa fedha na mali, imehusishwa moja kwa moja na ufisadi.
Huu ni uongo mkubwa, ni mbegu mbaya inayojegwa na adui, kutaka kurufisha nyuma maendeleo ya nchi.
Ukweli ni kwamba unaweza kufanikiwa kabisa huku ukiwa mwadilifu, ni rahisi sana kufanikiwa kihalali kwa mujibu wa sheria.
2. Wewe mwenyewe unahusika kwa asilimia mia moja( Your responsible for your life 100%)
Mwelekeo wa maisha yako kiuchumi unakutegemea wewe mwenyewe, hakuna mtu mwingine anaye husika
- Siyo jukumu la wazazi
- Siyo jukumu la kanisa
- Siyo jukumu la serikali au wanasiasa.
Hawa wote wanacho weza kufanya ni kukutengenezea mazingira mazuri tu, lakini hata kama ikitokea wameshindwa kufanya wajibu wao, basi huna sababu kwanini usifanikiwe, kwasababu  jukumu na uwezo wa kufanikiwa uko mikononi mwako 100%.
3. Kwenye mafanikio ya kiuchumi, kila kitu kinatakiwa kianze kwenye mawazo.
( Start with the end in mind)
Ubunifu au designing ya maisha yako kiuchumi, inaanzia kwenye mawazo yako.
- jua nini unataka
-Wapi unataka kuelekea kiuchumi
Lazima ujenge picha( the blue print) ya kile unachotaka kukijenga, picha hiyo lazima ijengeke kwenye akili yako, the designing must be done on your mind, wekeza kwenye hili eneo kujua hasa nini unataka na wapi unataka kuelekea/ kufika, the destiny must be clearly understood in your mind.
4. Jenga shauku ya kufanikiwa. ( Create desire to succeed).
Shauku ni driving force ya kukusukuma na kukuwezesha kuvishinda vikwazo vyote utakavyo kutana navyo njiani.
Safari ya kuelekea kwenye mafanikio ya kiuchumi ina vikwazo vingi, utakutana na sababu tisa za kukukatsha tamaa, moja tu ndiyo itakayo kutia moyo, hivyo usipokuwa na nguvu ya kukushikilia uendelee kuwepo, shauku ndiyo nguvu itakayo kushikilia. 
Kuna njia mbili zitakazo kusaidia kuijenga shauku ya kufanikiwa.
a) Kuuona mwisho tangu mwanzo.
Ukiipata picha halisi ya kule unako elekea, ukijiona wewe ukiwa tayari umeshafanikiwa kiuchumi, ukiweza kuyaona hayo maisha ukafanikiwa kuyavuta tangu mwanzo, shauku kubwa itajengeka ndani yako.
b) Ukijua sababu kwanini ufanikiwe( get to know your why?)
- Sababu itakufanya shauku yako ijengeke zaidi, na utavishinda vikwazo vyote.
5. Tengeneza mfumo utakao utumia kujenga mafanikio yako ya kiuchumi.
Ili uweze kufanikiwa kiuchumi lazima kuwe na mfumo ambao unautumia, hakuna mafanikio ya kiuchumi nje ya mfumo.
# Unaweza kutumia mfumo wa ajira/ Kuajiriwa
# Unaweza kutumia mfumo wa biashara/ kufanya biashara au kuwekeza kwenye miradi mbali mbali.
Ni swala lisilo ingia akilini wewe unataka kufanikiwa kiuchumi halafu hauko kwenye mfumo wowote, chagua mfumo mmoja wapo halafu stick kwenye huo mfumo na uufanyie kazi.
Toa muda wa kujifunza mfumo unaotaka kuutumia kujenga mafanikio yako ya kiuchumi.
Kama ni biashara anza kujifunza namna ya kufanya biashara.
* Hudhuria semina za ujasiliamali
* Soma vitabu vinavyo husiana na mambo ya biashara
* Jifunze kutoka kwa watu wengine wanaofanya biashara
*Soma majarida au magaazeti yanayo husiana na biashara
* Tafuta marafiki au network ya wafanyabiashara wenzako, anza kuhusiana nao, na jifunze kutoka kwao.
# Kama wewe unataka kupitia kwenye mfumo wa ajira, basi unaweza
* Kujiendeleza kielimu, ili uwe kwenye mazingira mazuri ya kupata ajira nzuri
* Unaweza uka volunteer, ukaenda short courses au ukafanya jambo lingine lolote litakalo kupa uzoefu utakao kusaidia kupata kazi.
6.  Personal Development.
Utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa kiuchumi, kama utajenga tabia ya kufanya personal development.
- Mabadiliko ya kimtazamo( Attitude change)
- Uboreshe namna yako ya kufikiri
- Baadhi ya tabia zako inabidi zibadilike.
Ukweli ni kwamba mafanikio yako, yawe ni ya kiuchumi au mengine yoyote, yatabebwa na 80% personal development na hiyo 20% iliyobaki ndiyo itakuwa ni hayo mambo mengine.
~Paul Masatu.
Previous
Next Post »