.

UKifanya Yale Ambayo Wengi Wameshindwa Kufanya Utapata Yale Ambayo Wengi Hawana.


 Na: MROPE wa MROPE
IMEKUPASA KUWA TAYARI KUFANYA YALE AMBAYO WENGI WAMESHINDWA KUFANYA ILI KUPATA YALE AMBAYO WENGI HAWANA.
Kama una ndoto za mambo makubwa lazima uwe tayari kufikiri, kutamka na kutenda mambo makubwa ambayo wengi hawajawahi hata kuyaota. Kwa kufanya hivyo lazima utarajie kuonekana upo tofauti na wengi wanaofikiri, kutamka na
kutenda mambo madogo madogo.
Gharama ya kufikiri, kutamka na kutenda tofauti na wengi na kuonekana mshamba, mkoloni, unajitenga, na mambo mengi ambayo hayaendani na wao.
Katika hali ya kawaida mtu mwenye ndoto kubwa hata akiongea ataonekana kama ana kichaa maana anaongea yale "yasiyowezekana" na anapita katika kanuni "zisizowezekana" na anapata matokeo "yasiyotarajiwa".
Katika hili lazima mtu akubali jamii imuone wa ajabu kidogo hasa katika nidhamu ya matumizi na hapo ndipo ubaya utakapoanza. Jamaa bahili, pesa zake zina masharti, mambo yake kama mzee n.k. Kubali hayo kwa kuwa umechagua njia tofauti na ukiamuamu kuwafurahisha wao maana yake njia unayoiendea imekushnda na umejiandaa kuwa wa "kawaida".
Si jambo jepesi kujinyima leo ili kutimiza malengo ya miaka 10,20,30...100 ijayo lazima uonekane "dish limeyumba". Wakati mwingine ili kujiweka mahali salama na usiyumbishwe na vyema kujiepusha na makundi na marafiki wanaofikiria nyama choma, hapo ni lazima utengwe nao na "ukazaliwe upya" katika kundi la watu wenye malengo makubwa.
Kwanini? Kwa sababu wewe ni binadamu na kuna wakati unarudi ktk uhalisia wa magumu yako leo unajiona unayopanga kutenda hayawezekani na ukikutana na marafiki "wa kawaida" watakuambia kuwa "katika siku ulizofikiri kwa usahihi ni leo ulipogundua kuwa una ' mipango kichaa"' na wewe utafarika na faraja ya kushindwa.
Kama una ndoto kubwa unahitaji marafiki ambao ukiwaambia umeshindwa watamani hata kukuwasha makofi, wawe wakali tena waongee mpaka povu liwatoke kwa "upuuzi" unaowaeleza.
Kama una ndoto kubwa chagua kuwa tofauti na wengi maana wengi hawana ndoto kubwa.
Cheers. Che Mrope Wa Mrope, Mbeba Maono (fb page) 0766656626/0787641417/0715366010
Previous
Next Post »