.

Salamu Kutoka Mapiramidi Ya Farao...!

Na: MROPE wa MROPE.

Leo ukipata nafasi ya kuzungumza wa wazungu na ukawauliza ni jambo gani linafanya waheshimu waafrika watakuambia ni nguvu nyingi walizonazo waafrika zilizowapa jeuri ya kujenga mapiramidi kule Misri. Historia inaeleza ujenzi wa mapiramidi haukuwa jambo la mchezo na ilihitaji kujenga na kujenga kwa miaka 20 mfululizo mpaka
kukamilisha mapiramidi hayo achilia mbali muda wa kuchoronga mawe toka katika miamba na kuyasafarisha mpaka huko "site". Inaelezwa kuwa watu wakichukuliwa kwenda "site" iliwapasa kufanya kazi ya ujenzi miezi mitatu mfululizo na wakianza kulegea wanarudishwa na kuletwa wengine kuendeleza ujenzi. Kwa ufupi kulikuwa na zamu ya kuhakikisha nguvu haikomi wala kulegea kwa miaka yote 20.
Wenzetu wale wanasema, "ilikuwaje waafrika wakamudu kuweka malengo yaliyohitaji zaidi ya miaka 20 bila kutetereka, kuhofia au kubadili msimamo? Ilikuwaje wakaweka malengo ya kutenda mambo makubwa hivyo wakiwa wana teknolojia duni jambo ambalo hata leo katika teknolojia kubwa duniani hakuna anayeota kujenga mapiramidi?".
Sio kama hayapendwi lakini shughuli yake ni pevu na wanaogopa kwanza hawaelewi wapi waanzie.
Kumbe dhamiri, maamuzi ya uthubutu na juhudi zikiingia kazini hakuna jambo ambalo haliwezekani, hakuna cha teknolojia duni wala kusingizia kuwa ni mawazo ya kiwendawazimu.
Kilichopo ni kuweka dhamiri kisha kutenda, kutenda, kutenda na kutenda zaidi mpaka kinaeleweka. Dosari ya watu wengi kushindwa kufikia malengo yao ni kutamani kutenda mara moja na kwa haraka kisha wapate matokeo.
Makosa ya wengi ni kutamani malengo yanayotimia ndani ya mwaka mmoja na ndio maana gari na jumba la kifahari ndio malengo yao makubwa.
Usisitishwe na mtaji mdogo wala usitishwe na historia nono ya umaskini wa ukoo wenu tena usitishwe na kutokuwa na midigrii kichwa na wala usihofie kutokuwa na ajira ya mihela mingi, inuka na ujenge mapiramidi yako bila kujali itachukua miaka mingapi ila cha msingi amua miaka mingapi mbele unataka ufike unakotaka kufika.
ALOYCE MROPE, Che Mrope Wa Mrope (fb) Mbeba Maono (fb page) 0766656626/078764147/0715366010
Previous
Next Post »