.

Mtu Aliyefilisika ni Rahisi Kurudi Katika Utajiri


Na: MROPE WA MROPE. Iringa

Kuna jambo natamani kuwashirikisha kwa kifupi sana.
Naomba niulize maswali haya: 1. Huwa unajisikiaje katika vionjo kama ulitarajia ule wali maini halafu ukafika mezani ukakuta ugali mchicha? 2. Unafanyaje kama huna
pesa lakini kuna mtu anakudai deni ambalo usipolipa litakushushia heshima? (unadaiwa kodi, unadaiwa na mkwe n.k) 3. Unajisikiaje ukifanya biashara unayotarajia upate milioni 10 halafu ukapata laki 8? Natamani kujua kabla na baada ya tukio kupita unajisikiaje? Natamani kujua hata aina ya msukumo unaojisikia ndani yako?
Naam mmegusa mahala nilitamani kujua kama binadamu wote wako hivyo.
Hapo ndipo safari ya wengi kuelekea kupata anachotaka huwa inakufa. Nitarejea kusema jambo kwa kifupi sana.
Kuna mambo mawili utayagundua kwa haraka 1. Kuna uhitaji mkubwa umejiwekea lakini umeshindwa kuufikia 2. Maumivu yatokanayo na mahitaji makubwa uliyojiwekea na hatimaye i. Kukata tamaa ii. Kujisuta kwa kupenda au kutarajia mambo makubwa iii. Kulaumu walio kufanya ufikiri ktk viwango hivyo vya juu
Kwa kawaida hiki ndicho kipindi halisi cha mtu kufanikiwa kwa sababu zifuatazo: 1. Unajikuta kama ni mtu mwenye deni
kutokana na kukosa ulichotarajia na hivyo utajikuta unahitaji kupata ulichokosa ili kuziba bajeti ulizopanga kupitia ambacho ungepata na hapo ukiinuka utapgana kwa nguvu sana kuliko mwanzo. 2. Kupitia jaribio la mafanikio yaliyofikiri bila shaka ulikutana na watu wengi muhimu kuhusu ulichokuwa unafanya na ni rahisi kuwatumia hao kuamka upya 3. Kukosa kule kutakuwa kumekuongezea umakini na mafunzo mengi kuhusu jambo ulilokuwa ukifanya 4. Akili yako ilishahamia ktk malengo na matarajio makubwa hivyo hata mwili ni rahisi kufuata iliko akili 5. Uzoefu unaonesha mtu aliyefilisika ni rahisi kurudi katika utajiri kuliko ambaye anaanza kwa mara ya kwanza. Kwa hoja hizo nakusihi uangukapo amka haraka usongee mbele ukalala na kugalagala utakanyagwa na wanaopita na ufe kabisa.  NINI KIFANYIKE ILI UAMKE? 1. Muombe Mungu akupe ujasiri 2. Epuka watu wasio na malengo watakuumiza na kukupoteza 3. Pata ushauri wa kisaikolojia/watu wanaojua kumtia mtu moyo na kuamka na morali kuu 4. Kaa karibu na watu waliopata kupata hasara au kupitia magumu na wakaamka. Itakusaidia. Ni hayo tu nilitamani kuwashirikisha nga kidogo baada ya kugundua ni tatzo sugu.
 
Previous
Next Post »