.

MNYORORO WA UTAJIRI...!


Na: Albert Sanga. Iringa
Ngoja niwape mchapo halafu nitaendelea kidogo. Jana nilikwenda mtaa mmoja hapa Iringa mjini unaitwa Wilolesi. Huko nilikwenda kutazama kiwanja ambacho kinauzwa. Nilipofika kule
nikaonana na bwana mmoja ambae huwa ninaonana nae mjini mara kwa mara; na ndie muuzaji wa eneo hilo. 

Kiwanja hiki alipewa na babu yake ambae alishafariki miaka ya nyuma. Alinieleza kuwa anakiuza sio kwa sababu nyingine isipokuwa anataka fedha ili akanunue nyumba nyingine huko Dodoma. Anyway, kilichonifurahisha ni historia ya eneo hilo. Alikuwa muwazi, kuwa babu yake alikinunua mwaka 1982 kwa shilingi elfu sita kutoka kwa mwenyeji mmoja. Leo hii anakiuza kiwanja hicho milioni 470! Nilichoka! Pointi ni nini hasa?....ni kwamba; kuna mambo ambayo ukiyatenda leo wajukuu zako watakuja kuchekerea, lakini kuna mambo usipoyafanya leo basi watoto na wajukuu zako watakuja kutukana kaburi lako na kuuliza ulikuwa unawaza nini wakati .

Nilipoishia nilitoa mfano wa Yesu Kristo uliohusu talanta, ya kwamba kuna ambae alipata talanta 5, mwingine 2 mwingine 1. Nikaeleza kwamba kuna mantiki ya makundi matatu ya watu katika mfano huo. Yaani wafanyakazi, wafanyabiashara na wale walio iddle a.k.a wasio na kazi...

Kwanza niwafahamishe kwamba ni kosa kiimani, ni kosa kijamii na tena ni kitokwenda sawa kwako binafsi kusema ama kudhani kwamba hakuna kitu cha kufanya, kusema hakuna fursa, kusema hakuna ajira, kusema mshahara ni mdogo na hata kudhani kwamba hakuna njia ya kutokea...

Kwa nini ni kosa? Ni kwa sababu Mungu alipoumba dunia hakukuwa na serikali hii ina maana alitaka ufanikiwe hata pasipo serikali. Kulalamikia serikali kutokukumbuka kwa ajira ama mshahara mdogo, itabidi upigwe viboko!...

Tuache hapo kidogo hebu twende kwenye wafanyakazi na wafanyabiashara. Usisahau kuwa tunaongelea mnyororo wa utajiri. Na ninarudi kwenye mfano wa talanta kidogo. Huyu investor alietoa hii mitaji (talanta) aliwaambia wale waliopewa kwamba wafanye biashara wazalishe faida. 

Nini kilitokea? Jamaa mwenye 5 akazalisha nyingine tano na jamaa mwenye 2 akazalisha nyingine 2 maana yake wali double mitaji, right?! Haya hebu tumcheki huyu aliepewa moja. Huyu jamaa aliepewa moja akaenda kufukia eti kwa madai kwamba talanta moja haitoshi kufanya chochote cha maana! Sikiliza mwenye talanta alichomwambia, akamwambia "ulishindwa kuweka talanta hii moja hata kwa watozao riba?" Usichoke ati na huu mfano, nakuja sasa kwenye pointi ninayotaka uinyake. Kwa lugha nyingine ni kwamba badala ya kufukia tu hela aliyopewa(ile talanta) ingekuwa jambo la maana angeiweka kwa hao watozao riba a.k.a benki. Ngoja nitokee hapa kukupeleka ninapotaka ufike. 

Hivi si unafahamu kazi ya benki? Okei, kazi ya benki ni kuwakutanisha wenye hela lakini hawana mawazo na wale wenye mawazo isipokuwa hawana hela; kwa kuwakutanisha huko benki inazalisha faida kupitia  alieweka hela benki na uthubutu wa aliekwenda kukopa benki. BENKI inampa nini anaeweka hela benki? Inampa kitu kiitwacho riba ambayo ni ndogo ukilinganisha na thamani ambayo ile hela inazalisha. 

Hebu pozi kidogo! Hebu rudi kidogo kwenye ule mfano wa talanta, halafu tujiulize swali: kwa nini yule bwana aliewapatia jamaa zile talanta hakuwapa option ya kuziweka hela benki(kwa watozao riba)? badala yake tunaisikia hiyo option mwishoni kabisa baada ya yule jamaa aliepewa talanta moja kushindwa kuifanyia chochote na kuifukia?
Hadi hapa tunaona kwamba kuweka hela benki ni kusema, "jamani.eheee mimi ni hela hapa ila nimeshindwa jinsi ya kuzitumia mimi kama mimi; hivyo naomba mnisaidie katika kufikiri namna gani zitumike".
Ukishawakabidhi, benki wanakupa masharti makali. Kwanza watakwambia ili tukupe riba fulani hela yako lazima ikae miezi mitatu, sita, tisa n.k. Yaani hata uwe na shida aje jamaa hawacheki na wewe, wanakula bati mpaka ule muda ufike. Kiufupi wanakuwa na urafiki na wewe unapoenda kuwapatia ila baada ya hapo wanaendelea kukunyanyasa mpaka utakapozitoa hela zako. Tupo jamani?....
Wengine wameshaanza, ohooo Sanga, unatuleta kwenye benki na wakati umesema unaongelea wafanyakazi nawafanyabiashara. Wangapi kati yenu mnafahamu kwamba neno talanta mbali na kumaanisha fedha pia linamaanisha kipaji/karama/uwezo/maarifa n.k?
Naamini wengi mnaelewa. Kwa hiyo unapokuwa na kipaji/karama/uwezo/maarifa; una machaguo matatu. 1) Kufanya biashara 2) Kuweka kwao watozao riba 3) Kufukia ama kukaa bila kufanyia chochote. Sijui mnanipata!? Ngoja nitoe mfano: ukisomea ualimu unakuwa umepata uwezo/ujuzi/ wa kufundisha, right? Basi hapo una options tatu: kuufanyia biashara ujuzi huo, kupeleka ujuzi wako kwao watozao riba ama kupotezea uwezo wako (kukaa bila kufanya chochote)......
Sasa tuje hapa. Unapochukua vyeti vyako vya ualimu na kwenda kutafuta ajira, maana yake ni kwamba umepeleka ujuzi wako kwao hao watozao riba! Yaani ni kwamba umeshindwa kufikiria cha kufanyia ujuzi wako hivyo umeona ni bora umkabidhi mwajiri afikirie namna atakavyotumia ujuzi wako, huku akikupa riba kidogo.
Riba ni mshahara na wote tunafahamu kuwa mishahara ni kasehemu kadogo ka thamani unayozalisha hapo kazini. Yaani wewe hauna tofauti na yule alieweka hela benki kwa miezi mitatu akilipwa riba ya asilimia 3 wakati benki wanazalisha faida ya asilimia 18 hadi 30 kupitia hela yako hiyo hiyo. Ujuzi wako, profeshno yako, umeamua kuikabidhi kwao hao watozao riba, a.k.a waajiri! Tunakwenda sawa?
Sasa nakuuliza swali la ufahamu. Unadhani ni kwa nini options ya kuweka talanta benki.haikishauriwa miaka 2000 benki. Kwa unadhani kuweka hela benki ni vibaya? wala hata sio vibaya! Ahaa, labda hujaelewa, je, unadhani kuukabidhi ujuzi wako kwa watozao riba a.k.a waajiri ni jambo baya? Akhuuu! wala sio baya! Lakini unajua kwa nini? Ni kwamba sio option ya kwanza ya mashujaa. Naomba niishie hapa kwa leo. Nitaendelea ili niconnect na ufanyabiashar, ufanyakazi na namna unavyotakiwa kutoka.
Sasa nakuuliza swali la ufahamu. Unadhani ni kwa nini options ya kuweka talanta benki. haikushauriwa miaka 2000 iliyopita?. Kwa unadhani kuweka hela benki ni vibaya? wala hata sio vibaya! Ahaa, labda hujaelewa, je, unadhani kuukabidhi ujuzi wako kwa watozao riba a.k.a waajiri ni jambo baya? Akhuuu! wala sio baya! Lakini unajua kwa nini? Ni kwamba sio option ya kwanza ya mashujaa kiuchumi. Naomba niishie hapa kwa leo. Nitaendelea ili niconnect na ufanyabiashara, ufanyakazi na namna unavyotakiwa kutoka. Asanteni sana kwa kunisikiliza, tuonane wakati ujao.

 
Previous
Next Post »