.

Maamuzi Yako Yanaweza Kubadili Maisha Yako...!

Na : MROPE WA MROPE  

Mafanikio au kutofanikiwa ktk maisha yako kunatokana na maamuzi unayoyafanya kila unapohitajika kufanya maamuzi. Kuna maamuzi ya kukuboreshea maisha yako unatakiwa kuyafanya haraka na kwa umakini mara unapohitajika kufanya maamuzi hayo maana ukichelewa utakuwa
umechelewa na mlango wa mafanikio utakuwa umejifunga kwa kuwa milango ya mingne hufunguka kdogo na kwa muda mfupi ukichelewa na kujisisita unajifunga. Hapa msisitizo wangu ni kufanya maamuzi makini na ya haraka.
Kuna wakati ni lazima ufanye maamuzi hata kama magumu na ya kuumiza lakini lazima ufanye ili ufike.
Ugumu wa kufanya maamuzi ya kipekee ni upweke maana ni wachache wanamudu kufanya maamuzi hayo hivyo utajikuta huna kampani ya wale uliowazoea na wale uliowazoea si ajabu wakawa maadui wa maamuzi yako.
Kwa hiyo kuna kufanya maamuzi na kusimamia ulichokiamua hata kama utaonekana kama chizi ulipoteza muelekeo na hii ndiyo inaitwa kulipia gharama ya mafanikio yako.
Kwa hiyo unahitaji umakini daima katika maisha maana maisha ni kuhusu uchaguzi wa maamuzi ya aina mbili; mazuri au mabaya, yanahuisha au yanayoangamiza, yanayoinua au yanayoshusha.
Jambo jingne ni kuwa maamuzi yanayohitajika kufanywa ili kupata mafanikio ni maamuzi yanayoogofya na yaliyojaa sonono kuu lakini imetupasa kupenya katika mlango ulio mwembamba ili kufikia mafanikio tuyakayo.
ALOYCE MROPE, Che Mrope Wa Mrope (fb), Mbeba Maono (fb page) 0766656626/0715366010
 
Previous
Next Post »