.

FIKRA CHANYA MWANZO WA MAFANIKIO


Na: MROPE WA MROPE. Iringa

MTU MWENYE FIKRA CHANYA HUONA VISIVYOONEKANA, HUGUSA VISIVYOGUSIKA NA HUPATA VISIVYOWEZEKANA. 

Kimsingi hakuna kisichowezekana, kisichogusika wala kisichoonekana kwa yeyote ambaye ana mawazo chanya. Kuwaza kwamba ninastahiki kuwa na hiki na kile na kile na hapa nilipo sipo mahala sahihi ninapostahili ni hatua muhimu sana kuelekea mafanikio. Kutazama kila jambo katika namna ya kiutendaji na kulifikia ni hatua muhimu. Kutazama (SOMA ZAIDI )
jambo katika kujipa visingizio na sababu murua za kutofanya ni kosa kubwa lakini kujidanganya kuwa umefika wakati hujafika ni kosa kubwa zaidi.
Mafanikio yanasukumwa na kuchoshwa na kutoridhishwa na pale ulipo. Hauwezi kusafiri kwenda mahala kama pale ulipo na mahala unapopapenda maana hutakuwa tayari kutoka na hata ukitoka utarudi mahala unapopapenda. Ni aibu kusema haiwezekani kwa jambo ambalo viumbe wengne kama wewe wanaweza.
Umeumbwa ukiwa kamili na mwenye akili njema kufanya mambo makubwa. Huwa inaleta maswali tunapomudu kufanya kazi za watu katika viwango vya ubora mpaka tunapandishwa vyeo na kusifiwa daima na wakubwa wetu wa kazi lakini katika mambo yetu tunaweka nguvu na akili ndogo na kushindwa vibaya.
Ina maana sisi tumezaliwa ili kutumikia wengine? Kama tunashndwa kujituma na kujenga mazingira ya kujijengea kipato cha kila siku au kila wiki na kusubiri pato la kila mwezi pekee ni dhahiri tunaweka matumaini yetu ya kufanikiwa katika kushndwa.
Tunatumia kila siku na kusubiri kinachopatikana kinachopatikana mara moja kwa siku 30 ili kutumia kila siku ni kulazimisha kuona tumefika wakati hatujafika.
Mazingira yoyote ya kuridhika na hatua uliyonayo sasa ni kujiaminisha kuwa wewe haustahili zaidi ya hapo na ya kwamba uwezo wako umefika mwisho. Mahitaji yetu ni kila kona, kila muda na kila mahala katika nyakati tulizopo duniani na zile ambazo hatutakuwepo.
Tumesikia watu wakisema, "kama baba na mama wangekuwepo nisingepata tabu". Mimi nasema kama baba na mama wangetazama mbele na kuacha ubinafsi wa kujitafutia kinachowatosha wao tu na wakati mwngne hakiwatoshi kusingekuwa na tabu hizi.
Kumbe maisha mazuri na bora kwa vizazi vyetu hayawezekani kwa kuwa tumekataa kuona kisichoonekana, kugusa kisichogusika na kuweza yasiyowezekana. Bado umeridhika?
ALOYCE MROPE, Che Mrope Wa Mrope (fb) Mbeba Maono (fb page) 0715366010/0766656626/0787641417


 
Previous
Next Post »