Na: MAKIRITA AMANI
Changamoto ya kila mtu kwenye dunia ya sasa ni muda. Hatuwezi kupata muda wa kutosha kufanya kila kitu tunachopanga au kutamani kufanya kila siku.Na hii inaleta umuhimu wa kuweka vipaumbele.Sasa leo
tafakari hivi;
NI VITU GANI VITATU TU ambavyo kama ukiweza kuvifanya
leo, vitaleta mabadiliko makubwa kwenye kazi yako, biashara yako na
maisha yako kwa ujumla?
Angalia vitu vyote ulivyopanga
kufqnya leo, chagua vitatu tu, na vipe muda wa kutosha kwa kuanza
kuvifanyia kazi leo. Usiguse kitu kingine kabla hivi vitatu havijaisha.
Hebu anza hili leo kama jaribio tu, halafu ona ni jinsi gani litaongeza ufanisi wako.
Hebu anza hili leo kama jaribio tu, halafu ona ni jinsi gani litaongeza ufanisi wako.
UWE NA SIKU NJEMA SANA.
Sign up here with your email