.

Ujasiriamali Siyo Kusaka Pesa tu...!


Na : MROPE WA MROPE. Iringa
SALAMU ZA MWISHO WA WIKI: Ujasiriamali sio kusaka pesa tu kama wengi wanavyofikiri. Ujasiriamali ni uwezo wa kutumia fursa yoyote kujipatia mafanikio. Fursa zenyewe ni kila jambo linalokuja mbele yako bila kujali ni baya au zuri maana matukio lazima yaendelee kutukia katika uhai wetu wote lakini hakuna guarantee ya
kupata matukio mazuri tu hata mabaya yatatokea.
Hata mabaya hutokea hata kama unaomba na kusali sana maana wakati mwingne mema hutanguliwa na yale tunayofikiri ni mabaya. Ayubu alipata kuwa mtu tajiri zaidi kuliko mwanzo baada ya watoto wake wote kufa, mali zake zote kuteketea na yeye kupgwa majipu mwili mzima.
Muda wake wa kuugua aliutumia kulia, kuomboleza na kumuadhimisha Mungu (ulikuwa wakati mgumu kwake lakini alitumia muda ule kama fursa ya kumkaribia Mungu badala ya kulalamika), Daudi kabla ya kuwa mfalme aliwekwa huko machungani, kazi ambayo walifanya watu wasiofaa lakini ilikuwa ni njia ya kuandaliwa kuvaa joho la ufalme.
Yusufu aliuzwa na nduguze lakini ilikuwa ni fursa ya kuishi jumba la kifalme. Akiwa kwa falme akasingiziwa ubakaji akapelekwa jela lakini ilikuwa ni njia kuelekea uwaziri mkuu. Musa alitupwa na mama yake lakini ilikuwa fursa ya kulelewa kifalme. Kwa hiyo itoshe kunielewa kuwa kuna mafanikio yanakujia kupitia matatizo lakini kanuni inataka usimame imara katika matatzo hayo na uone fursa uchangamkie au utulie tuli ukitafakari na sio kulalamika.
Katika salamu zangu hizi kwako nataka uelewe kuwa unapaswa kufahamu kuwa ujasiriamali ni pamoja na kugeuza mabaya kuwa mazuri. Yawezekana una msongo wa mawazo na ikifika saa 7 usingizi unakata unaishia kujigeuza mpaka alfajiri. Mbeba maono nakushauri utumie fursa hiyo. Kuna watu wanatamani kuamka muda huo na hawawezi kuamka kwa uchovu, wewe kukosa usingizi ni bahati njema. Tumia muda huo jisomee mbinu za mafanikio kupitia vitabu, mitandao n.k.
Tumia muda huo kumuomba Mungu na ujue uwezo mkuu wa kutenda mambo makubwa ulioumbiwa na Mungu. Tumia muda huo kutafakari namna ya kubadili maisha yako. Natamani kukuona ukibadili matatizo kuwa faida. Natamani matatizo yakuone wewe ni mbaya wake kuliko matatzo. Kukosa usingizi iwe fursa isiwe matatizo na wewe utakuwa shujaa.
Muda huo wa kukosa usingizi ukifanya hayo utagundua hata wewe unafurahia kukosa usingizi maana ni faida. Mwisho wa kukosa wewe utakuwa umefaidika na sio kuharibika kama wengine wanavyoharibikiwa. Salamu zako kwako ni kutaka uwe mjasiriamali unayetumia kila fursa ikiwepo matatizo kujinufaisha. Hizo ni salamu zangu mwisho wa wiki kwako.
ALOYCE MROPE, Che Mrope Wa Mrope (fb), Mbeba Maono (fb page) 0766656626/0715366010/0787641417

 
Previous
Next Post »