.

When I Want To Know Something, I go for It...Huwezi Kujifunza Kilimo cha Maparachichi Kwa Kusoma Kitabu

 
Meshack Maganga : Iringa. Go Big Or Go Home. 

When I want to know something, I go for It. And only on rare occasions I take a secondhand opinion.
Nilimpigia simu Rich Dad wangu wa Mafinga kumuomba Muda wa kwenda kujifunza zaidi, kilimo hiki. Nilifuatana na Baba yangu kabisa (Mzee Maganga alisafiri kutoka nyumbani kwetu Sumbawanga.
Tulifika shambani kwa Rich Dad. Kwenye shamba la
Miparachichi lililopo Mafinga. Tofauti na wakulima wengine na pengine binadamu wengine, mzee huyu anafanya mambo kisasa, Ni mkulima asiyekurupuka. Na ana maarifa hasa, Anasoma vitabu vingi na majarida ya kilimo kila siku. Kiukweli nilishangaa sana, wakati baadhi ya watu wanaona chupa za maji kama ni uchafu mkubwa wa kutupa huko kwenye dustbin, yeye anakusanya hizo chupa na kuzichimbia kwenye pembeni ya shina la Mparachichi na kutoboa mfuniko wa chupa kidogo.
Maji yanawekwa kwenye hiyo chupa na yanadondoka taratibu wiki nzima. Kwa hiyo mparachichi unapata maji muda wote. Kiangazi chote. Wakati watu wengine wanalalamika maji ni shida kuna mzee huku anapeta, anazidi ku fanikiwa na kufundisha wengine.
Na hapa yana miaka miwili tu na yameshaanza kutoa maua. If you can visualize your goals, even if they are just a few short - term ones at the start, then there's a strong probability that you can achieve them.
Penda unachokifanya tena sana tengeneza brand yako. Ukipata nafasi panda mti kwenye eneo lako.
Na uchaguzi unabakia mikononi mwako. Go Big Or Go Home. The Choice is up to you nobody else
Previous
Next Post »