Na: Albert Sanga--Iringa
Yesu Kristo alisema, "Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake, na
mengine yote mtazidishiwa". "Pattern" (sio context) ya falsafa hiyo
inaweza kuwa "applied" kwenye uchumi, kwamba, "Tafuteni uwekezaji kwanza
na vitega uchumi na kisha hayo mambo yanayohitaji matumizi
mtazidishiwa".
Unajua ni kwa nini watu wengi wanafeli kiuchumi?
Ni kwa
sababu wakipata fedha jambo la kwanza wanafikiria matumizi badala ya
uwekezaji na vitega uchumi. Wanakimbilia kununua mavazi, kujenga nyumba
za kuishi, kununua magari ya kutembelea, kumiliki simu za gharama,
starehe, n.k.
Mwanzo hufurahi lakini muda si mwingi baadae wanagota.
Lakini ukipata fedha, (iwe ni mkopo, iwe umepewa, iwe ni umejiwekea
akiba, iwe ni mshahara n.k), ukianza kwa kuhangaikia uwekezaji na vitega
uchumi basi uwe na uhakika kwamba mengine yote, (kama magari ya
kutembelea, nyumba za kuishi, mavazi makali n.k) utazidishiwa.
Unapowekeza, mwanzoni unaweza kuonekana kama unaechelewa ama
ukachukuliwa poa ama ukaonekana hauendi na wakati; lakini utakapoanza
kuvuna uwekezaji wako; kila mtu lazima atakupa saluti! Ukianza kwa
kutumia usithubutu kujilinganisha wala kucheza karibu na mtu alieanza
kwa kuwekeza, unaweza kujiona mjaja sasa lakini muda si mrefu unaweza
ukaumbuka. ~SmartMind~
Meshack Maganga---Go Big Or Go Home
Sign up here with your email