.

FAHAMU MAZINGIRA YA BIASHARA...!





Na: Paul Masatu

Kwenye makala hii napenda kuzungumzia mazingira ya biashara(business environment) ambayo ni vizuri kukusanya taarifa zake ili ziweze kukusaidia kabla ya kuanzisha biashara yako.
Na mazingira haya ni mazingira ya
jamii ambayo mjasiriamali anakusudia kuanzisha biashara yake.
Ni muhimu sana kwa mjasiliamali kupata taarifa za jamii ambayo anakusudia kuanzisha biashara yake.
Utafiti huu wa jamii hiyo ambayo anakusudia kuanzisha biashara yake unaitwa "Community demographics" taarifa hizi zitamuwezesha mjasiliamali kupata picha kamili ya uwezo wa hiyo jamii kufanya manunuzi, mjasiliamali anaweza kuangalia mambo mengi kutoka kwa hiyo jamii ili kuweza kupata taarifa hizo, kwenye makala hii nimekusudia kuweka mambo machache. Ambayo ni HALI YA KIUCHUMI YA JAMII HUSIKA, AINA YA WATU.

#1. Hali ya kiuchumi ya jamii hiyo.( Economic base of the community)
Kwenye eneo hili mjasiliamali atatakiwa kupata taarifa ya hali ya kiuchumi au kimapato(level of income) ya jamii husika, hapa unaangalia hali ya ajira kwenye jamii husika, hii ni muhimu kwa sababu ndiyo inakupa picha ya uwezo wa kifedha wa hiyo jamii, na kutokana na uwezo huo utapata pia picha ya wapi matumizi yao makubwa yalipo, hii kwa ujumla wake inakupa picha ya nguvu ya manunuzi( purchasing power) ya jamii hiyo.
Chukulia mfano wa jamii labda ya manzese na mbezi bichi, kwa kuangalia kipengele kimoja tu cha income level, kinaweza kukupa taarifa muhimu ya aina ya biashara unayoweza kuanzisha kwenye jamii husika. Mfano biashara kama super markets, malls au biashara yeyote ya vitu vya thamani, unapata picha ya awali kabisa ya wapi kati ya maeneo hayo mawili panafaa kuanzisha biashara hiyo. Au duka la nguo za thamani, kwa kigezo cha mapato, utapa picha ya wapi uanzishe biashara hiyo kati ya Sinza na Tandika.
INAENDELEA..






















Meshack Maganga---Go Big Or Go Home
Previous
Next Post »