By Elizabeth Samoja
Baada ya kuwaona waafrica tukiwanyenyekea sana watu wa ngozi
nyeupe nilikuwa nikidhani wao kunavitu vya ziada mungu kawapendelea...baada ya
kukua,kusoma elimu ya darasani,na baadae kuwekeza muda wa kutosha kusoma vitabu
vya mafanikio na biblia nikagundua kuwa wanadamu wote ni sawa Tatizo la
mwafrica kunakitu hajakigundua ndo maana anaendelea kuwa alivyo leo...
Watu wote ni
sawa,watu wote wanatabia
zinafanana..majungu,wizi,ulevi,roho mbaya,roho nzuri,kupenda
anasa,etc...vithibitisho..Biblia hebu soma tabia ambazo zinakemewa ndani ya
kitabu kitatifu....tabia mbaya zote zimekemewa...Je kitabu hicho kiliandikwa na
mwafrica???? hicho ni kithibitisho number moja......
Number mbili toka nimeanza kusoma vitabu vya success
kunatabia waandishi wanazikemea kama chanzo cha kufanya watu wasisonge mbele
ikiwa ni uvivu,kutokujiamini,kutojiandaa,kutokupa elimu ya kina juu ya jambo
unalotaka kulifanya na mengine mengi...vitabu hivyo vingi vimeandikwa na mzungu
kwa kuangalia mazingira yanayowazunguka.....lakini ukweli waafrica katika hili
nalo hawapo nyuma...wamejaa hofu,hawathubutu chochote,hawako tayari
kujifunza,wanachukulia mazungumzo ya vijiweni na kukomalia utafikiri yanatokana
na utafit etc....
Kunakitu ambacho mungu alificha maarifa yote ndani yake na
ambao tu wataweza kupangundua ndo wataifurahia dunia hii,lasivyo wengi tutakuwa
tumekuja duniani kusindikiza maisha....na wenzetu wajanja walijaribu kukifanyia
utafiti na kukipata huku wakimwomba roho mtakatifu awaongoze nacho ni POWER OF
SUBCONSCIOUS MIND .....hapa ndo panapoleta tofauti.....usipoirisha vizuri hii sehemu
ya ubungo wako....kwisha habari....shetani nae analijua hili...ndo maana
kawakamata watu katika eneo hili pia.......Waafrica wengi wanaamini katika
uchawi na kwamba nguvu za kiza ndo kila kitu....yupo kazini na hirizi,anaenda
kanisani na hirizi,kila mwisho wa mwaka anamwaga damu makaburini na kuomba
mizimu kinyume na mpango wa mungu...kwa kufanya hivi na kuendeleza haya yote
vizazi na vizazi mfumo mzima wa subconscious mind unaharibika na kuamini mambo
yasiyo ya msingi na kuuwa uwezo wake wa kukuwezesha kufikia mambo ambayo mungu
alikuumba kuja kuyafanya hapa duniani......
Sisemi kwamba ngozi nyeupe hawapo wanaoamini katika
uchawi.ila africa imekuwa kero kiasi kwamba mtu hafikirii chochote..kila gumu
akikutana nalo anahisi uchawi.....pia hajafunguka upande wa pili wa jinsi ya
kuimentor subsconcious mind yake......kitu chochote ukikirudia zaidi ya mara 21
moja subconscious mind inajua ni kweli...ukirudia kusema uongo fulani zaidi ya
mara 21 unaifanya system yako kuamini hivyo,ukienda kwa waganga kila unapokutana
na tatizo subsconscious yako inaamini uganga ni kila kitu........hivyo kuuwa
uwezo wako wa kufikiri kinyume na hapo
Mungu si mganga wa jadi...ila wengi wanataka awe mganga wa
jadi....ndo maana kanisa litakalotangaza miujiza ya kumiliki nyumba na gari kwa
muda mfupi litapata waumini wengi haraka sana....kwasababu watu hawa bado nguvu
za giza zimewakamata na kuamini katika mafanikiko ya haraharaka kupitia
mtumishi huyo mganga wa jadi aliyekuja kwa njia ya kujifanya ni mtumishi wa
mungu........
Sasa nini kilichotofautisha mwafrica na mzungu?.....Kabla
sijaongelea itambulike kuwa hata wazungu si kama tunavyowafikiria....kuma
pareto rule inasema hivi 80/20 kwa maana hiyo mafanikio makubwa tunayoyaona kwa
wazungu yameletwa na asilimia 20% ya wazungu....wengine ni followers
tu.....sasa kama ndo hivyo....asilimia 20% africa nayo ikichukua jukumu hili
tutafika mbali sana sana...si lazima kila mtanzania ama mwafrica alete
mabadilikoa africa...wachache wenye fursa zao wangezitumia vizuri kama wenzetu
walivyofanya tungefika mbali sana na pasingekuwa na mwafrica kumuona mzungu
kama mungu....bali wangekuwa watu tu kama sisi.....mfano kunavyuo vingi
tunakimbilia kusoma huko nje vilianzishwa na watu binafsi kama sehemu ya
kupunguza mapungu yaliyo katika mfumo mama...kwani sisi tunashindwa nini???
Ubinafsi au? kila mtu anajiwazia yeye na watoto wake tu au?....
Shetani anakiri sana anajua fika juu ya kazi ya sadaka na
kila roho inayopokea sadaka inafanya kazi sawa sawa.....mfano ukitoa sadaka kwa
mganga wa kienyeji yale mapepo yanaletwa maishani mwako na kuongoza maisha yako
na yana nguvu kweli na utaona mafanikio uliyoyaomba....sema shetani alivyokuwa
mjanja zaidi hakuweka shariti gumu sana mfano fungu la kumi ambalo limeonekana
kuwa tatizo kwa wengi.....mtu anayeingiza mil 100 ukimwambia atoe 10% anaona du
10mil zote ziende church si mtumishi atanenepa sana....ila mganga yeye hanahaja
ya 10% ukimpa tu hata mil moja na ng;ombe unaendelea
kubalikiwa.......hahahahhaha...
lakini pia shetani akawa mjanja zaidi...anakupa na matokeo
moja kwa moja ili akukamate ipasavyo.....Lakini ukweli ni kwamba ukielewa aina
za sadaka,kazi za kila sadaka na mashariti yake kwa upande wa mungu hakuna
linaloshindikana...biblia inamifano mingi ya watu waatiifu ambao mumgu
aliwainua sana sana...........Shetani bado mjanja tu...hata akupe mali lazima
mwisho wa siku akuaibishe tu.....na mara nyingi mali zake huondoka na
aliyezizalisha na anamashariti ya kijinga sana kukupima kama wewe unaakri
timamu au la.....mfano anakwambia nitakupa kila ktu ila ulale chini,usivae
viatu,ulale na mama yako,ulale na dada yako etc...hapa anakupima tu....Mungu
wetu hanamasharti ya kijinga maana anajua mtu aliyemuumba ni wa thanmani sana
na anatakiwa kufurahia utajri wake akiutengeneza kwa njia nzuri
Ukilijua neno litakuweka huru na hapatakuwa na haja ya
kumnyenyekea mzungu,mzungu anatakiwa kuwa partner tu na si kwamba yeye ndo kila
kitu....Kunakazi ya ziada inahitajika kufanyika africa ili kumkomboa mwafrica
kifkra...
Wazee wetu kama akina mandela,nyerere walitumia muda wao
hapa duniani kuhakikisha sisi ngozi nyeusi nao tunaoneka huru na kutambulika
duniani...sasa tunahitaji akina nyerere wengine na si lazima wawe wanasiasa
ambao wamepata fursa ya kulijua hili nao waweze kuplay their
part.....tusiendelee kunyamaza,tuendelee kupambana kumkomboa mwafrica katika
ukoloni mamboleo...
Kwa kuwa sasa kila kitu kipo wazi wazi sababu ya
globalization tuwasome wenzetu,tujipange wakija kushituka wanakuta hatuhitaji
mikopo yao na misaada yao ambayo inaendelea kutufanya watumwa kwao.....hivi
tuchukulie wewe ni mzazi halafu bado unamuhudumia kijana wako mwenye miaka 50
kama mtoto hii ni kweli jamani? Tuzindukeni.....unajua kwanini mandela
alifanikiwa? alienda england kusoma law na akawa mwafrica kwa kwanza kuanzisha
law firm....katika masono hayo yalimwezesho kugundua kitu cha oppression ndo
akaja akaanza mapambano....unatakiwa kumjua adui wako kwa kina then unaandaa
mkakati wa kupambana nae.........Mungu ibariki Africa,Mungu Ibariki
Tanzania.....bado tunahitaji ukombozi,na ukombozi huu utaletwa na sisi
wenyewe,hao wazungu usidhani wanapenda ukombozi wetu kiuchumi...wao wanapenda
madini yetu,gesi zetu n.k kwa sababu wameshatusoma wakatuona hola...na wao
hawaandani madhara ya miaka 3-5 wao wanaandaa madhara ya miaka 50 hadi mia.....so
mwanzoni mwa msaada utanona raha ila mwishowe ni machungu...................
Wako katika ujenzi wa taifa la leo na la kesho
Elizabeth Samoja
Meshack Maganga---Go Big Or Go Home
Sign up here with your email