Na: Meshack Maganga - Iringa. Go Big
or Go Home
Ndugu
zangu, juzi ijumaa nilikuwa kwenye maongezi ya kawaida na Dada yangu, mwalimu
na mshauri wangu Dada SUBIRA, ambae
ndiye mmiliki wa Blogu ya WAVUTI.
Tulikuwa kwenye maongezi ya kifamilia, kisha nikamshirikisha harakati zangu za
ufugaji wa samaki, akapata hamasa, akaniomba niwashirikishe na Watanzania
wenzangu kwa maandishi. Na mimi nikakubaliana na ombi hilo. Unaweza
kufanikiwa sana tu, unaweza kuwa billionaire ama milionea. Chunguza marafiki
zako na watu unaoshinda nao waliofanikiwa, jifunze kwao na
usipojifunza
utaendelea kuwa mlalamikaji.Fursa ya ufugaji wa samaki, kilimo cha miti, kilimo
cha nyanya na vitunguu ishakudondokea, usijjite myonyenge, ama maskini maana ‘victim
mentality isn’t going to get you anywhere’ GO BIG
OR GO HOME.
Ninachokiamini
katika maisha yangu ni kwamba, kila mtanzania anayonafasi kubwa sana ya
kuendesha maisha yake ya kila siku bila tatizo endapo atajitambua na kuugundua
ukuu wa Mungu ndani yake. Mwanadamu yeyote anaetambua uthamani wake na bahati
aliyopewa na Mungu ya kuendelea kuishi na kuzaliwa Tanzania hawezi kuishi
maisha ya kubangaiza.
Katika
Makala yangu ya wiki hii ningependa kuwashirikisha kitu kidogo sana nacho ni UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MAZINGIRA YA
KIJIJINI KWA MTAJI MDOGO SANA… kipindi cha nyuma, nilikuwa nikiwaona
watanzania wenzangu hasa huku Iringa, wakijishughulisha na ufugaji wa samaki,
ni miaka miwili imepita sasa, lakini nilikuwa ‘bize’ na mambo yangu sikutaka
kujifunza Zaidi kuhusu fursa hii. Mwanzoni mwa mwezi wa nane (8) mwaka jana
2014 rafiki yangu Nicolaus Kulangwa,
ambae huko nyuma alinifundisha kilimo cha Matango,alinipigia simu akinitaka nikataembelee mradi wake wa kufuga
samaki. Nilienda kijini kalenga hapa Iringa. Nilichokiona nilianza kukifanyia
kazi hapohapo na siku ileile. Wakati rafiki yangu akiwa na jumla ya mabwawa
saba ya samaki aiana ya sato na pelege mimi ndio kwanza nilijutia muda ambao
niliambiwa kuhusu fursa ile halafu nikazembea kuifanya.
Kama
tunavyofahamu, lengo la uajasirimali ni kupata faida ya unachokifanya na kugusa
jamii inayo mzunguka mjasirimali. Na kama ilivyo kwa mifugo mingine yeyote ile,
kabla ya kuanza kufuga kuna mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa ili ufugaji
wako uweze kuwa tija iliyokusudiwa na hivyo kufikia malengo ya mfugaji huyo.
Lakini kutokana na mazingira ya ufugaji wa huku Iringa hasa Kalenga, nitayataja
mambo hayo kwa kifupi sana, mambo haya huenda yakatofautiana kutoka eneo moja
la nchi hadi jingine, na kwa vile mimi sijasomea chuo cha ufugaji wa samaki,
maelezo haya ni yale niliyoyapata kwa uzoefu tu, siyo ya kufundishwa chuo, mapungufu
yatakayogundulika na ‘wasomi’ wataniandikia email ili nikawashirikishe
wenzangu.
Mambo hayo ni kama ifuatavyo:
ENEO
AMA SEHEMU YA KUWAFUGIA SAMAKI.
Inasisitizwa kwamba, eneo hilo liwe na udongo mzuri ambao hautaruhusu
maji kupotea hovyo. Udongo wa mfinyanzi ni mzuri na iwapo eneo lako lina udongo wa tifutifu ama
udongo wake ni kichanga unashauriwa kujengea kwa simenti ama kuweka ‘kapeti gumu’
lisilo ruhusu maji kupotea.
UPATIKANAJI
WA MAJI,wote tunafahamu kwamba samaki huiishi majini, maji ndiyo roho ya
masaki, samaki ni maji na maji ni samaki. Hivyo eneo la kufugia lazima liwe na
maji ya kutoshana salama kwa kipindi cha mwaka mzima. Vyanzo vya maji kwa ajili
ya ufugaji wa samaki ni kama chemichemi, mito, maziwa na maji ya ardhini hasa visima Kwa maeneo ya huku Iringa,
tunabahati ya kuwa na mto Ruaha ambao maji yake yapo muda wote wa kipindi chote
cha mwaka. Inashauriwa kwamba eneo hilo liwe salama ili kuwalinda samaki na
mfugaji kwa ujumla.
BWAWA.
Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na eneo
la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina
gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada
na wenye tija.
MBEGU
AMA VIFARANGA, mfugaji wa samaki anashauriwa kutembelea maeneo ambayo wafugaji
wakubwa wanazalisha vifaranga ili aweze kupata mbegu bora anayohitaji. Kwa
wananaoishi Iringa na maeneo ya jirani, wanaweza kupata mbegu kwa bwana Nicolaus.
UTUNZAJI
WA BWAWA NA USAFI. Ili mfugaji aweze kunufaika na miradi ya kufuga samaki ni
lazima uafanye usafi wa kutosha ndani nan je ya bwawa lake. Hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu
na viumbe wengine kama konokono,vyura, nyoka, na kenge wasiweze kufanya makazi
na hatimaye wakawadhuru samaki. Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara moja.
ULISHAJI.
Tofauti na mifugo mingine kama kuku, samaki hawahitaji kula chakula kingi sana.
Katika hatua za mwanzo ulishaji wake unaweza kuwa mara tatu kwa wiki ama Zaidi.
AINA
YA CHAKULA. Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya
pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa, Karanga zilizosagwa, unga wa mahindi,
mabaki ya chakula kama ugali nk.
Kuna
mambo mengi sana ya kuzingatia unapaanza kufuga samaki, mambo mengine ni kama
vile kuzingatia miiundo mbinu, wafanyakazi, kuzingatia masoko, utaalamu nk.
CHANGAMOTO
KATIKA SAMAKI ni magonjwa kama vile magonjwa ya samaki yapo mengi yakiwa nayasababishwa
na vimelea vifuatavyo magonjwa yanayosababishwa na bakteria, magonjwa
yanayosababishwa na virusi magonjwa yanayosababishwa na minyoo, magonjwa
yanayosababishwa na protozoa. na magonjwa yanayotokana na lishe duni.
Chanagamoto nyingine ni kama vile, Tatizo
mojawapo ni la kuvuja kwa kuta za bwawa. Tatizo hili hutokea iwapo ujengaji wa
bwawa haukufuata maagizo na taratibu za ujengaji wa bwawa. Kuna ndege, kenge,
fisi maji, nyoka hutokea. Iwapo bwawa lipo mbali na makazi. Kudumaa kwa samaki
kutokana na kuwa wengi bwawani kupita idadi inayotakiwa.
UVUNAJI
WA SAMAKI. Hujudi za mfugaji ndio zinaweza kupelekea kuvuna samaki wa kutosha
na kumletea faida kwa muda mfupi. Wakati wa kufaa kuvuna samaki bwawani
hutegemea ukuaji na aina ya samaki. Ukuaji wa samaki pia hutegemea ubora wa
chakula. Samaki wanaofugwa katika bwawa lenye hali nzuri watakuwa tayari
kuvunwa baada ya miezi 6 hadi 8. Kuna watakao sema huu ni muda mrefu, ukiona
ufugaji wa samaki wanatumia muda jaribu kingine. Ama endelea kukaa nyumbani
kwako, ukiisubiri serikali na mashirika ya kijamii yakusaidie.
Nielezee
kwa kifupi jinsi ufugaji wa samaki unavyochangia ajira binafsi kwa watanzania
na faida yake kwa ujumla. Changamoto mbalimbali za kiuchumi, na ukosefu wa
ajira kwa wasomi wanaotoka vyuo vikuu kwa sasa, imesababisha watanzania wengi
kuanza kuwa wabunifu na kuanza kujishughulisha na ujasiriamali hasa kilimo na
ufugaji. Kwa sasa mabwawa mengi yanapatikana katika mikoa sita yenye rasilimali
nyingi kama Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma. Ufugaji wa
samaki umeenea kote nchini.
Kwa
sasa kilo moja ya samaki huuzwa shilingi 7,000/ kwa huku Iringa na ukiuuzia
bwawani kwa jumla ni shilingi 4000/ kwa kilo. Hii ina maana kwamba ukiwa na
kilo mia 7 za samaki una uhakika wa kuwa na milioni mbili na laki nane kila
baada ya miezi sita, kama utauzia bwawani kwa bei ya shilingi elfu 4 kwa kilo
ambapo hii ni samaki watatu tu aina ya sato, je ukiwa na samaki ama kilo elfu
tano? Utagundua kwamba adui wa mafanikio yako ni sentensi za kizamani ulizo
weka kichwani kwako.
Niseme
wazi tu kwamba, ufugaji wa samaki, ni fursa nyingine ambayo ipo wazi kwa kila
Mtanzania kuifanya, kuna watakao singizia mitaji, hali ya hewa nk,lakini ukweli
ni kwamba bwawalangu dogo nilitumia pesa ndogo sana kulichimba ikiwa ni pamoja
kununua vifaranga vya samaki.
Tumekuwa
watu wa kujiwekea mipaka ya mafanikio vichwani mwetu. Kumbuka kwamba ukishajiwekea
mipaka ya mafaniko. Maisha yetu yataweza kubadilika iwapo tutabadilisha namna
tunavyoyatazama mambo. Kwa mfano unaweza kuwa umejiwekea mipaka ya kimapato
kwamba wewe mwisho wako ni kupata laki moja, mtazamo huo ukikaa kichwani basi
ukiambiwa bwawa moja linaweza kukutolea shilingi milioni 25 kwa miezi sita,
utakataa na hivyo fursa hiyo itakupita.
Nilipokuwa
nikisoma kitabu cha ‘THE TRUTH SHALL
MAKE YOU RICH’ Cha reallionaire mdogo kuliko wote Farrah Gray kwa sasa,
nimejifunza kwamba, maisha yetu yanaweza kubadilika muda wowote na dakika
yoyote iwapo tutajijengea Imani kwamba, maisha yanawezekana popote. Na kwa
Tanzania hii ambapo kila mwananchi anaruhusiwa kulimiliki ardhi kwenye mkoa
wowote umasikini litakuwa ni swala la kujitakia.
Ninamalizia
makala hii kwa kusema kwamba, kila saa katika maisha yetu ni fursa, makala hii
pia ni fursa kwako na kwangu, kuna baadhi ya nchi duniani ambapo wananchi wake
hawana bahati ya kukaa kwenye meza zao na kujifunza mambo haya. Kwawatakao
penda kuja Iringa, kujifunza ufugaji wa samaki, tunawakaribisha sana. Nicolaus na mimi na wafugaji wengine
watakusaidia kuapata elimu Zaidi yahii niliyoandika hapa.
“MY MOTTO IS GO BIG OR GO HOME”Binadamu wote wenye mafanikio duniani
hawachoki kutafuta..! MAWASILIANO. meshackmaganga@gmail.comhttps://www.facebook.com/pages/Fresh-Farms-Trading
Sign up here with your email