.

MABADILIKO vs MAENDELEO


Na: Mwl‬ Makwaya

Karibia kila mtu anapenda na anahitaji maendeleo lakini sio kila mtu anapenda mabadiliko. Watu wanapenda kufaulu mitiani yao, kufanikiwa katika biashara na mipango yao, katika kila wanalofanya wanapenda kuendelea.Lakini hakuna maendeleo mazuri kama hakuna mabadiliko. Kwa mtindo huu wa kupenda maendeleo bila kuyahusisha mabadiliko wengi tumeishia kuendelea mdomoni kwenye vitendo tupo pale pale.
Unataka
kuendelea kwenye biashara yako zaidi ya hapo ulipo lazima ukubali baadhi ya mabadiliko inaweza ikawa ni kwenye matangazo au ni kwenye kuwalipa mishahara mizuri wafanyakazi wako au inaweza kuwa ni kubadilisha mashine za uzalishaji nk lakini ni lazima ukubali mabadiliko kadhaa wa kadhaa yatakayokuletea maendeleo. 

Ukiwa muoga wa kukubali au kufanya mabadiliko basi usiwe mwepesi wa kulilia maendeleo. Cha muhimu usibahatishe katika kufanya mabadiliko maana raha ya mabadiliko mengi hua inaonekana mapema hiki kimeshachoka ngoja nikibadilishe.

Kama vile makocha wa mpira ambapo wakiwa wanatafuta ushindi lakini wanaona hawapati huanza kwa kuwaita wachezaji pembeni na kuwapa maelekezo nini cha kufanya. Lakini pale wanapozidi kuona mambo ni magumu hufanya mabadiliko na wakati mwengine mabadiliko wanayofanya mashabiki hua hawayakubali ila mabadiliko hayo yanapoleta ushindi kila mmoja humuona kocha mzuri. Sio kwamba hua wanafanya mabadiliko kwasababu hawawapendi wachezaji wanaofanyiwa mabadiliko laa ila wanapenda maendeleo na maendeleo yao ni ushindi. Sasa basi wewe ni kocha wa maisha yako mwenyewe kama unataka ushindi lazima ukubali mabadiliko.

Ni ukweli usiopingika mabadiliko mengi ya maendeleo hua ni magumu kufanya lakini kama unataka maendeleo ni lazima uyafanye. Mfano huichukua serikali kuvunja na kulipa nyumba za kandokando mwa barabara ili kupanua barabara hizo. Ni rahisi kusikia timu fulani imetimua kocha na kuleta mwengine ili timu yao ipate kombe. Baadhi ya makampuni hubadilisha hata uongozi wa juu kabisa ili wafanye vizuri katika soko. 

Mabadiliko ya marafiki
Mabadiliko ya vyanzo vya taarifa
Mabadiliko ya aina ya vyakula
Mabadiliko ya aina ya Vitabu
Mabadiliko ya aina ya usomaji
Mabadiliko ya masaa ya kulala
Mabadiliko ya jinsi ya kuweka akiba.
Mabadiliko ya jinsi ya kumwabudu muumba
Mabadiliko ya jinsi ya kuishi katika mahusiano yako.
Mabadiliko ya nini cha kufanya na nini si cha kufanya.
Mabadiliko ya wapi pa kwenda na wapi si pa kwenda.


Hayo yote yanaweza kukufanya ukapiga hatua kubwa ya maendeleo kama utapatia katika kufanya mabadiliko.


Changamoto kubwa ya kukufanya mabadiliko ni kwamba watu wengi wamelizika na maisha waliuonayo hivyo hawawezi thubutu kufanya mabadiliko. Lakini kuna wakati unakuja ambao mazingira yanakulazimisha ukubali mabadiliko usisubiri wakati huo maana mabadiliko yake hua yanagharimu sana.
‪#‎Mwl‬ Makwaya#
©TO BE IS TO DO
Previous
Next Post »