Na: Albert Sanga- Iringa.
Jana nilisafiri kutoka Iringa
mjini kwenda kijiji kimoja kiitwacho Ndorobo, umbali wa kilomita takribani
170(kwenda na kurudi). Hapo nilifika kuonana na kijana mjasiriamali na
mpambanaji hasa; aitwaye Herry. Kijana huyu ana miaka 24; baada ya kumaliza kidato
cha nne matokeo yake yalikuwa mabaya, akaamua kurisiti pia matokeo yakagoma.
Akaona asiendelee kupoteza muda
kusumbukia "vyeti vinavyogoma"; akaamua kwenda kwa
mtu kujifunza ujuzi wa kuprinti t-shirts na mabango. Alipoiva kwa ujuzi huu akachukua "muvu" ya kijasiriamali. Kwanza akazunguka katika shule mbalimbali za huko vijijini akiomba tenda ya kuprinti t-shirts na kugongesha mihuri kwenye mashati. Akapata tenda kwenye shule mojawapo(kwingine hawakuweza kumwamini mapema); changamoto ikawa ni ukosefu wa mtaji.
mtu kujifunza ujuzi wa kuprinti t-shirts na mabango. Alipoiva kwa ujuzi huu akachukua "muvu" ya kijasiriamali. Kwanza akazunguka katika shule mbalimbali za huko vijijini akiomba tenda ya kuprinti t-shirts na kugongesha mihuri kwenye mashati. Akapata tenda kwenye shule mojawapo(kwingine hawakuweza kumwamini mapema); changamoto ikawa ni ukosefu wa mtaji.
Anasema alikuwa na simu yake
akaamua kuiuza kwa shilingi elfu 45 kisha akaenda kununulia t-shirts chache, na
materials ya kazi. Akaanza kidogo kidogo, akaanza kupata faida, sifa zake
zikaenea mahali pengi; na sasa ana tenda katika vikundi vya vikoba, ma-saccoss,
na mashule zaidi ya hamsini.
In short ni kwamba anavuna hela!
Faida aliyoikusanya akaipeleka kwenye biashara ya mashine za kusaga na kukoboa
alizonazo katika vijiji vitatu tofauti; na pia ana mashamba ya mpunga ekari
nyingi.
Na sasa anajiandaa kuagiza mtambo wa kisasa wa
kuprintia na kuchapishia kutoka China. Amejenga nyumba na ana viwanja vingine
vitatu Iringa mjini; yote akiwa na umri wa miaka 24 na bado anaishi zake
kijijini. Kuna masomo 15 nimejifunza kutoka kwa kijana Herry, lakini hapa ngoja
nikushirikishe matatu: 1) Kusoma ni kuzuri lakini kama hukubahatika kusoma ama
kama akili ya darasani huna; usipoteze muda kunung'unika ama kurisiti miaka
nenda rudi; jaribu mambo mengine; kwa sababu kutoka kimaisha hakupo katika
kusoma pekee! 2) Suala la kudhani unashindwa kufanya biashara kwa sababu huna
mtaji, hebu lifikirie upya kwa sababu hata Simu Yako Unayotumia Ni Mtaji Tosha
unaoweza kukutiririshia ‘ulakionea’ na hata umilionea 3).
Watu wengi wakishapata
"vielimu" ama wanaotafuta maisha; wamekariri kwamba kutoka kimaisha
kupo mjini. Uhalisia ni kwamba mjini kila mtu ni mjanja na fursa nyingi
zimeshatwaliwa; wengi wapo mijini ila wanasindikiza wengine; vijijini kuna
fursa nyingi na rahisi. Ni suala la ku-tune tu mtazamo wako. ~SmartMind~
Sign up here with your email