Na: Hadija Jabiri –
Iringa
Wengi tuna hamu
kubwa ya kufanikiwa maishani. Kati ya sababu ambazo hutufanya tusifanikiwe ni
pamoja na kukata tama tunapokuwa kwenye safari ya
mafanikio. Ili uweze kufanika
kwenye maisha katika enoe lolote (biashara, ndoa, dini nk) lazima uwe mtu
usiyefahamu maana ya neno kukata tamaa. Mafaniko ni sawa na barabara yenye kona
nyinyi, milima na mabonde na si njia nyoofu kama wengi wanavyofikiria. Ni rahisi sana kwa mtu kuianza safari ya
mafanikio lakini wengi huwa tunaishia njiani pale tunapoanza kukutana na
changamoto za safari.
Kati ya sababu
zinazoweza kumfanya mtu akate tamaa ni pamoja na ushauri, sina maana ya kuwa ni
vibaya kupokea ushauri toka kwa watu, lakini kubwa ni kulitafakari kila
unaloshauriwa na kuchukua lile unaloona lina msingi kwako, tunapaswa kufunga
masikio yetu ili tusisikie kabisa maneno ya kutukatisha tamaa.
Bila shaka huu
ni wakati muafaka kwako kuanza kusema hivi, Kama jambo ninalotaka kulifanya au
ninalolifanya lina manufaa kwangu na naamini litakuwa na mafanikio mbeleni,
kama jambo hilo halimchukizi mungu na kama jambo hilo halipinzani na sheria za
nchi basi nitalifanya na sitasikiliza maneno ya watu wanaojaribu kunikatisha
tamaa.
Tunapaswa kuwa makini sana na aina ya watu
tunaowaomba ushauri pale tunapotaka kufanya jambo Fulani au tunapokutana na
changamoto kwenye jambo Fulani. Ni vyema sana pale tunapotafuta ushauri juu ya
jambo Fulani kuwafata watu waliofanikiwa kwenye jambo hilo.
Sababu nyingine
inayokatisha wengi tamaa ni kushindwa, ikiwa kama mtu alijaribu jambo Fulani na
akawa na matarajio makubwa ya kufanikiwa basi ikitokea hakufanikiwa kama
alivyotarajia hukata tamaa kabisa na hata kiogopa kufanya tena.
siamini kama kushindwa kunatakiwa kukukatishe
tama, kushindwa ni moja kati ya vitu vya msingi unapotaka kufanikiwa, baada ya
kushindwa hupaswi kukata tamaa au kuogopa kujaribu tena na badala yake
unatakiwa kukaa chini na kujiuliza sababu gani haswa zilipelekea ushindwe
kufikia mafanikio na wakati mwingine unapofanya jambo hilo tena basi unalifanya
kwa ustadi zaidi. mfano Kama umeweka lengo la kufika Dar es saalam ukitokea
Makambako kwa usafiri wa gari moshi na ukaambiwa njia ya gari moshi imeharibika
basi panda basi au ndege, mwisho wa siku hakikisha unafika Dar na si
kughairisha safari kwasababu tu njia ya gari moshi imeharibika.
Waliofanikiwa
wameshindwa mara nyingi sana.
Thomas Edison aliyegundua taa ya umeme alifanya majaribio zaidi ya elfu tisa
kabla ya kufanikiwa, Donald trumph ambaye nimwekezaji mkubwa kwenye majengo
nchini marekani alishafilisika miaka ya tisini lakini hakukata tamaa na sasa ni
mmoja kati ya watu wenye nguvu kubwa nchini Marekani. Je Thomas Edson angekata
tamaa leo tungekuwa na taa za umeme? Na kama Donald trumph angekata tamaa leo
dunia isingeziona Trumph Towers? Hivyo moja kati ya sababu kubwa
zinazowatofautisha waliofanikiwa na wasiofanikiwa ni uwezo wa kuinuka baada ya
kuanguka. Waliofanikiwa wanatabia ya kuendelea kwenda mbele bila kujali
wameanguka mara ngapi wala ubovu wa njia wanayopita.
Kumbuka, Mtu
yoyote hawezi kukukatisha taama juu ya jambo lolote bila ridhaa yako. Jiamini
na amini unaweza kupata chochote unachokitaka maishani mwako. Tupo mwanzoni
kabisa mwa mwaka 2015, fanya uamuzi leo na anza kuzifuata ndoto zako kwa gharama
yoyote bila kuwasikiliza wakatisha tamaa.
’’ Your life
is your choice’’
Sign up here with your email