.

KUWA MTOTO TENA:- Naamini ni swali ambalo watu wengi wanajiuliza na kukosa majibu.







  Na: Hadija Jabiry- Iringa Tanzania

Kwa miaka mingi nilikuwa nikijiuliza swali hili ‘’Nitawezaje kufanikiwa kwenye maisha?’’ Naamini ni swali ambalo watu wengi wanajiuliza na kukosa majibu. wengi tunatamani kuwa na mafanikio makubwa kwenye maeneo mbalimbali maishani lakini hatupati majibu ya nini haswa tunatakiwa kufanya ili kuweza kufanikiwa .

Kwangu pia ilikuwa ngumu kupata majibu mpaka nilipoanza kuitwa mama, kwa kumuangalia mwanangu, watoto wengine wanaonizunguka na kwa kusoma historia za watu waliofanikiwa niligundua ili kuweza kufanikiwa maishani tunataakiwa kufanya kitu kidogo sana na kitu hicho ni , ‘’KUWA WATOTO TENA’’
Zifuatazo ni baadhi tu ya tabia walizonazo watoto na ndizo tabia za watu waliofanikiwa kwenye maeneo mbali mbali maishani.

NDOTO KUBWA, wengi tunakumbuka ukubwa wa ndoto zetu za utotoni, watoto wengi ukiwauliza ukubwani wanataka nini watakwambia kuwa marubani, maraisi , madaktari na nk. Ndoto zao zote ni kubwa, na vivyo hivyo ili kufanikiwa lazima urudi utotoni na kuanza kuota ndoto kubwa, ndoto ya bill gate ilikuwa kila nyumba na ofisi duniani iwe na kumpyuta na ikumbukwe kuwa aliota ndoto hiyo wakati ambao wengi waliamini hilo haliwezi kutokea.

WATOTO SI WAOGA, ili uweze kufanikiwa lazima uwe na ujasiri wa kutenda, moja kati ya sababu zinazopelekea wengi tunashindwa maishani ni uoga, mara nyingi hatujaribu kkwasababu tunaogopa kushindwa, mtoto haachi kujifunza kusimama au kutembea kwa kuogopa kuanguka , bill gate hakuwa mooga na ndio maana aliweza kuacha chuo na kuingia kwenye biashara, ujasiri wa kutenda ndio uliomfikisha hapo alipo leo

WATOTO HAWAKATI TAMAA,mtoto haoni shida kukuomba kitu hata zaidi ya mara kumi mpaka ahakikishe anakipata anachokitaka, tabiaa hii ya kuto kukata tamaa ndiyo waliyonayo wengi waliofanikiwa maishani, wengi waliofanikiwa walisshindwa mara nyingi sana kabla ya kufanikiwa na hawakukata tamaa.
Watoto wanatabia ya kufata wanachokita na si kukaa kusubiri wanacholitaka kiwafuate.

Hizo ni baadhi tu ya tabia chache walizonazo watoto ambazo kama tukiziiga basi tunaweza kufikia malengo yetu maishani.
Previous
Next Post »