Na: Meshack Maganga- Iringa.
Ndugu zangu, awali ya yote ninapenda kuwashukuru
Watanzania wote,walionipigia simu na kunitumia ‘sms’ nyingi sana baada ya
kipindi cha AMKA NA BADILIKA, kipindi ambacho kimewasaidia watanzania wengi
sana, kwa kubadilisha mitazamo. Nilipokea simu nyingi sana na wengi wa watanzania
hao walipenda kujifunza cha kilimo cha miti na mboga.
Wito wangu sikuzote umekuwa ni
kutumia muda wangu mwingi kuwasisitiza rafikizangu, ndugu na wadau wengine wote, kuangalia uwezekano wa kuzitambua fursa mbalimbali zilizopo kwenye mazingira yetu. Hakuna sehemu yeyote ya dunia ambayo haina fursa na ambayo imesahaulika, bila kuwa na fursa za kuitosha jamii, isipokuwa macho yetu ya ndani hayazioni fursa hizi. Vitakchubwa tuliyonayo ni ya kupambana katika kuondoa mitazamo hasi iliyomo kwenye vichwa vyetu tuweze kuziona fursa hizo.
kutumia muda wangu mwingi kuwasisitiza rafikizangu, ndugu na wadau wengine wote, kuangalia uwezekano wa kuzitambua fursa mbalimbali zilizopo kwenye mazingira yetu. Hakuna sehemu yeyote ya dunia ambayo haina fursa na ambayo imesahaulika, bila kuwa na fursa za kuitosha jamii, isipokuwa macho yetu ya ndani hayazioni fursa hizi. Vitakchubwa tuliyonayo ni ya kupambana katika kuondoa mitazamo hasi iliyomo kwenye vichwa vyetu tuweze kuziona fursa hizo.
Tumezungukwa na fursa (Neema ya Mungu) ni ajabu
kumsikia mtu anaeishi Morogoro ama Iringa halafu hafahamu kilimo cha vitunguu,
hafahamu kama kuna kilimo cha mitiki, ama haamini kwamba kuna watu wameshafikia
kwenye kilele cha mafanikio kwa kujishughulisha na kilimo cha matembele,
ufugaji wa samaki na mambo mengine madogomadogo ambayo waliopitapita vyuoni
wanadia kwamba ni hizo ni kazi za watu duni waliokimbia ‘umande’. Mtu anaishi
Dar hana taarifa kwamba Bagamoyo ama
Mkuranga, kuna kilimo cha mitiki, Vitunguu, nyanya, mihogo nk. Ajabu yingine kuna wanaoishi Iringa,
lakini hajawahi kujifunza kilimo cha
miti angalau wapande hata nusu ekari ya miti na huyu bado atakuwa anaitupia serkali lawama kwamba haimjali, swali,
unataka serkali ikujali wakati unalala na kushinda facebook kupiga majungu?
Badilisha mtazamo wako.
Watalaamu wa Elimu ya utambuzi na mawazo ya kina kama
akina Paul Msatu wanasema kwamba, Sisi sote ni mawazo yetu, kuishi kwetu ni
mawazo yetu, mafanikio yetu ni mawazo yetu, uchumi wa taifa letu ni mawazo
yetu.Utamaduni wa taifa letu ni mawazo yetu. Ukweli wa maisha yetu, mafanikio
yetu, upo ndani yetu katika mawazo yetu.
Uwezo mkubwa unaotutofautisha kati yetu sisi na viumbe wengine upo
katika mawazo yetu. Tabia zetu, matendo yetu, kuamini kwetu na zaidi kuishi
kwetu ni kuwaza kwetu. Mafanikio yote
duniani, utajiri wote duniani na hata umaskini wa mwanadamu vyote vimeanzia
katika mawazo na mitazamo yake juu ya maisha.
Hakuna
mtanzania asiyefahamu matumizi ya miti, labda kwa kukumbushana tu, baadhi ya
matumizi ya miti ni kama vile, mbao, nguzo, chakula, kilimo mseto, hifadhi ya
vyanzo vya maji, kurutubisha udongo, kulisha mifugo, kuboresha hali ya hewa, kuni,
mkaa, dawa na mapambo.
Kosa tunalolifanya na kusababisha tuzipoteze fursa za
mafanikio, hata kama zinachukua muda mrefu ni mtazamo mbaya wa kufikiri kwamba
fursa za mafanikio zipo nje ya maeneo tunayoishi. Ifahamike kwamba, fursa za
mafanikio ya kiroho na kimwili hutafutwa kwasababu haziwezi kujileta kwasababu
zina tabia ya kujificha. Baadhi ya fursa hujileta zenyewe kwetu na kama haziji
upande wetu ni vizuri tukazifuata kwenye maeneo yanayotuzunguka.
Kuna watanzania ambao wanafikiri upandaji wa miti ya
mbao na nguzo ni mkoani Iringa pekee, ninapenda kutoa wito kwa watanzania
wenzangu kwamba unaweza kupanda miti popote pale ulipo, (Tanzania Tree Seed
Agency- TTSA) wametoa mwongozo wa upandaji miti kwa kila kanda, na kila mkoa,
hakuna mkoa Tanzania ambao hakuna miti. Ukiwa Mwanza, Singida, Mbeya ama Kigoma
na kwingineko panda miti inayostawi eneo hilo na faida yake utaiona. Faida ya
miti huonekana baada ya miaka mingi 8-10 na kama huwezi kusubiri miaka hiyo ni
bora ufanye jambo jingine.
Ili kupata faida za miti hakuna budi kufanya uchaguzi
sahihi wa miti ya kupanda kwa ajili ya matumizi yaliyokusudiwa. Mfano miti
inayofaa kwa kivuli ipandwe sahemu zinazohitajika kuwa na kivuli na iwe ni ile
isiyopukutisha majani yote msimu wa kiangazi, miti ya kilimo mseto iwe ni miti
yenye mizizi inayokwenda chini zaidi ya sentimeta 50 na iwe inayorutubisha
ardhi, yenye kivuli chepesi na inayofaa kwa malisho. Miti ya mapambo iwe na
maua ya kuvutia, isiwe na mizizi inayotambaa mbali na isiwe inapukutisha majani
yote wakati wa kiangazi.
Hakikisha kuwa unapata mbegu bora za miti kwa ajili ya
kuzalisha miche ya kutosha kupanda katika maeneo utakayoyaandaa. Mbegu hizi
bora za miti zinapatikana kutoka Wakala
wa Mbegu bora za miti (Tanzania
Tree Seed Agency- TTSA). Ni Wakala wa Serikali ya Tanzania ambao ni idara iliyo
chini ya Wizara ya Mliasili na Utalii. TTSA ina uzoefu katika takinolojia ya
mbegu bora na safi za miti. Wakala pia unatoa mafunzo ya muda mfupi (majuma 2)
yanayohusu uvunaji mbegu hasa kwa wale ambao hawawezi kununua mbegu kutoka TTSA,
Wakala wa mbegu.
Kitalu
hujengewa banda ili kuwe na kivuli kwa mbegu zinazoota. Kibanda kinaweza kuwa
cha majani au fito zenye kipenyo cha sm 2 yaliyoshonwa kwa kamba kiasi cha meta
2 juu ya kitalu kwa kukiegemeza kwenye nguzo zilizofungwa pamoja na fito. Pande
zote za kitalu ziachwe wazi ili hewa ipite kwa urahisi.
Inapendekezwa na baadhi ya watalamu wa kilimo cha miti
kuwa - wakati miche michanga imeanza kuota majani ya kwanza, yango’lewe kwenye
vitalu na ipandikizwe kwenye viriba kama ifuatavyo: kishimo kirefu zaidi kuliko
mizizi ya miche kitengenezwe kwa kijiti ili mizizi isije ikapinda kuelekea juu.
Pia kishimo kiwe na upana wa kutosha, vinginevyo mizizi ya pembeni itashika
ukingoni na kupinda juu wakati mche
ukiingizwa.
Gharama ya kuanzisha bustani ya miche inatatofautiana
kulingana na mahali bustani ilipo. Ifahamike kwamba, unaweza kuanzisha kitalu
cha miche popote ulipo Tanzania, kuna wanaofikiria kwamba, uanzishaji wa kitalu
cha miche lazima iwe Iringa, ama Lushoto, Morogoro ama Njombe,unachotakiwa
kukifanya ni kubadilisha mtazamo. Wale wanaoishi Dar mtakuwa mmeshaona baadhi
ya watanzania wenzetu pembeni mwa barabara wakiuza miti, ukiwa na akili ya
kutoona mambo huwezi kuwaona.
Ninakuhakishia popote pale ulipo unawezakuanzisha kitalu
na ukauza miche, ikakuweka mjini. Kwa
upande wa Iringa hasa kijiji tunachofanyia kazi sisi, gharama ya kuanzisha
bustani yenye miche 100,000. Inakadiliwa kufikia shilingi milioni 4, hii
inajumuisha, gharama za udongo kutoka
mstuni, viriba, dawa za kuzuia wadudu, vifaa vya kujengea kitalu, mbao,
misumari, vifaa vya kufanyia kazi, kama vile matoroli, mipira ya maji, watering can, majembe nk. Mbengu, na
usimamizi kwa miezi mitano na banda la ofisi.
Miche huwekwa chini ya kivuli kama kile cha kitalu cha
mbogamboga.na umwagiliaji wa maji hufanywa mara kwa mara kutegemea na hali ya
hewa ya sehemu kitaulu kilipo.
Muda wa
kupeleka miche shambani unapokaribia
kivuli huondolewa polepole aidha kw kupunguza majani kwenye kibanda au kwa
kuondoa kibanda kwa muda mrefu zaidi kila siku mpaka miche itapoweza
kustahimili jua la moja kwa moja. Upunguzaji wa unywesheaji, dhidi ya mahitaji
ya miche itumike ili “kukomaza” miche tayari kwa kupanda shambani. Viriba
visogezwe mara kwa mara ili mizizi inayojitokeza chini ikatike. Njia nyingine
ni kuinua viriba na kukata mzizi mkuu
chini kwa kutumia kisu kikali. Viriba vinaweza kupaliliwa kwa kutumia
kijiti chenye ncha kali au kutumia mkono. Miche hiyo huchuka miezi 4 na
kuendelea kuikuza tangu siku ya kuipandikiza kutegemeana na miti inayohusika.
Uandaaji wa kitalu cha miche, unatakiwa ufanywe kwa
makini sana, usipokuwa makini utaotesha miche isiyokuwa na tija, ukumbuke
kwamba, uuzaji wa miche inaweza kuwa moja ya njia rahisi sana ya kujipatia
kipato popote pale ulipo, kwa mfano, kama umeotesha kitalu cha miche 5 (elfu
tano) ya mbao, kuni,dawa ama nguzo ama miti ya mapambo na kati ya hiyo miche ukabahatika kuuza miche
elfu tatu kwa bei ya shilingi mia tu utakuwa na uhakika wa kuvuna shilingi laki
3, na kwanini upate laki tatu wakati unaweza kuongeza ukubwa wa ndoto yako
ukapata zaidi ya laki 3? Ikumbukwe kwamba, wakati utakapokuwa unasubiri kuuza
miche na pengine kuipanda kwenye mashamba yako utakuwa unajishighulisha na kazi
nyinginezo kama bustani ya mboga nk.
Maadui wakubwa wa miti ni pamoja na magonjwa, wadudu,
moto na wanyama baada ya kuipanda. Adui mwingine wa kilimo cha miti ni mawazo
yetu, mawazo mgando yasiyotaka kuvumilia, ukipanda mti hasa ya mbao, nguzo nk,
usitegemee kuvuna baada ya mwaka mmoja, ni baada ya miaka 8 hadi kumi. Kama utaona
miaka 8 ni mingi usifanye hiki kilimo hakikufai. Tafuta fursa nyingine.
Ikumbukwe kwamba, mafanikio yanatokana na mawazo au
wazo la mafanikio. Wazo linatengeneza fursa na kama utabuni wazo jipya kwenye
mazingira yako utaibuka kuwa mshindi. Fursa za mafanikio zina gaharama yake,
kuna gharama ya muda, gharama ya pesa, na kama haupo tayari kulipia hizo
gharama hizo fursa zitakupita. Uchaguzi unabakia kuwa wako. “MY
MOTTO IS GO BIG OR GO HOME”
Binadamu wote wenye mafanikio
duniani hawachoki kutafuta..!
https://www.facebook.com/pages/Fresh-Farms-TradingMeshack Maganga 2014
Sign up here with your email