Na: Meshack Maganga- Iringa.
Nilipoandika
makala niliyoipa kichwa cha USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA NCHI YA
TANZANIA, Nililezea jinsi ambavyo watanzania wanaweza kutumia fursa zilizopo
kujiondoa kwenye umasikini wa kujitakia na pia kuacha tabia ya kulalamika sana
bila kuchukua hatua. Katika makala ile, nilipata mwitikio mkubwa sana. Kwanza,
nilipigiwa simu nyingi na kutumiwa barua pepe nyingi, baadhi ya wasomaji
walifunga safari na kuja Iringa ili kujifunza kilimo cha miti, na
baadhi yao waliamua kununua mashamba na wengine walinunua mashamba yenye miti kabisa.
baadhi yao waliamua kununua mashamba na wengine walinunua mashamba yenye miti kabisa.
Baadhi ya
wasomaji walinitumia ‘meseji’ wakiuliza, ‘hayo unayo andika ni kweli unayafanya
ama ni kilele tu? Kuna mmoja wa wasomaji
wa makala ile alinipigia simu na kusema wewe Maganga, umri wako na hayo
unayoyafanya mbona haviendani? Nilimjibu
kwamba maendeleo hayafuati rangi ya mtu, umri, ama umbo, maendelea yaweza
kwenda kwa mtu yoyote kama akiamini. Zaidi ya hayo niliwaomba wote walionipigia, wakipata muda wanitembelee
Iringa kujifunza kisha wachukue hatua.
Albert
Sanga, ameandika makala yenye kichwa kisemacho KAMA UNA
AKILI YA MATOPE; UTAKUWA NA MAISHA YA UDONGO amegusia wa kifupi sana jinsi
ambavyo nilivyoanza kilimo cha mboga na miti kwa mtaji wa shilingi 25,000/
ninajua kwa mawazo ya kawaida ni vigumu sana hasa kwa wale walipopita vyuoni na mashuleni kwa ujumla kuamini kile
kinachosemwa, lakini ukweli ndio huo, niliweza kwa sababu kichwa changu
kiliamini kwamba ninaweza...sikuwa na muda wa kulalamika, wala kuilaumu serkali
wama wazazi wangu. kwa sasa nimefanikiwa kukuza mtaji wangu na kununua mashamba
yangu mengi sana unaweza kunitafafuta nikakupatia ushuhuda wangu.
Vifafa vya
kiuchumi, ama kufulia husababishwa na mambo mengi sana, badhi ya sababu za
vifafa vya kiuchumi ni pamoja na Kufanya mambo bila kufikiria na kupata ushauri
wa kile unachotaka kukifanya iwe ni biashara ama ajira.Pia kuna wanao fahamu na
wamezisikia fursa mbalimbali lakini bado wanasubiri muda ufike (waiting for the
perfect moment) huenda wakaendelea kuusubiri muda muafaka mpaka watakapo zeeka. Kuamini na kutegemea ajira pekee kwa kuiona
ajira kama ndio muarobaini wa kutatua matatizo ya kiuchumi pekee yake na kukaa bila kujishughulisha.
Nimeishi
Iringa kwa muda wa miaka 9 sasa, nikiishi kwa kaka yangu ambae ni mjasiriamali
wa kuigwa, wakati ule mwaka 2007 alikuwa akinifundisha uwekezaji kwenye aridhi
na mashamba, kusema ukweli nilikuwa sielewi sana, niliona ni kazi kubwa pia kushinda shambani
ama kupanda miti kisha kuisubiri kwa miaka mitano ama saba, ninadhani
sikumwelewa kaka yangu kwasababu nilikuwa na akili za ‘KICHUO’ chuoni nilikuwa
nikipewa hela na ziliniweka kwenye black markets nikajisahau, nilipofika mwaka
wa pili nilisoma kitabu maarufu duniani
kiitwacho ‘RICH DAD POOR DAD’ kitabu hiki kilinihamasisha sana na kubadilisha
mtazamo wangu kuhusu maisha, ni mwaka huo nilipoanza kuwekeza kwa kununua
shamba la ekari tano wilayani Mufindi, nilipomaliza chuo nikajikita zaidi
katika kujifunza kutoka kwa kaka yangu Baraka, rafiki yangu Albert Sanga na Rich Dad wangu wa Mafinga ambae ni
mwenyekiti wa wapanda miti mkoa wa Iringa. Msomaji atakae penda kujua zaidi
nipo wapi kwa sasa anitafute.
Kuna wale
ambao wameamua kuitegemea serikali kabisa kwa kila kitu, wanaamka asubuhi, wanaoga,
wanapata kifungua kinywa, wanaelekea vijiweni kucheza karata na kucheza ‘pool’
asubuhi mapema bila kuwajibika, hawazalishi matokeo yake ni vifafa vya
kiuchumi.
Kuufikia
mafanikio si rahisi kutokana na nguvu za
nje zinazoweza kukufanya usahau haya kama uvivu, ujinga, kutosikiliza ushauri
kwa waliofanikiwa, kutokuwa na mshauri (mentor) anayefanya yale unayotaka
kuyafanya, uoga, kutojifunza mambo mapya, kuwa na marafiki wanaosema ponda mali
kufa kwaja, kupokea ushauri wa ‘bure’ kutoka kwa ndugu na marafiki ambao
wanaamini kwamba ujasiriamali ni kipaji na kwamba ni kazi ya waarabu, wahindi,
wachaga, wakinga ama wazungu peke yao.
Na kama
bado una imani kwamba ni wajibu wa serikali, mbunge wako maarufu, au kiongozi
wako maarufu wa chama cha siasa ukipendacho ambacho unakipigania usiku na
mchana, mpaka unakosa muda wa kufanya mambo yako binafsi au kama umeweka mawazo
kichwani kwako kwamba, mabadiliko ya katiba mpya yatasaidia kufulia kwako,utakuwa
unapoteza muda wako, na kwa hakika utakuwa unavikaribisha vifafa vya kiuchumi
maishani mwako.
Au, kuwa
na watu lukuki na watumiaji wa mali zako
nyuma yako (people behind you) na utamaduni wa kuyachukulia mambo kama yalivyo
kana kwamba ni utaratibu tu au utamaduni wa bora liende ili mradi kumekucha na hasa
ukosefu wa nidhamu katika maisha wa kufikiria siku kwa siku au wiki kwa wiki (
thinking day to day or week to week).
Usije
ukashangaa siku ya mwisho wa dunia unaulizwa na Mungu, swali kama hili,
ulitumiaje muda na rasilimali watu na
kipawa chako kwa muda wote wa
wamaisha yako ulipokuwa Tanzania? utajibu nini? utakata rufaa au
utatafuta wakili wa kukutetea? Fikilia chukua hatua za kuanza kuwekeza
taratibu.
Kumbuka kuwa haukuletwa duniani kulala,kushabikia mambo yasiyokuwa na
maana, au yasiyokuhusu, au kuwa mwanaharakati wa harakati zisizokuwa na kichwa
wala miguu, au kutuwama kama maji machafu shimoni.Au kuishi maisha ya ujanja wa
mbuni wa kuficha kichwa chake kwenye mchanga huku kiwiliwili kikiwa nje. Wewe
ni kiumbe cha pekee kinachotakiwa kubadilika kila siku kimwili,
kiakili,kifikra,kiuchumi,kiutamaduni,kiroho
na hata kiuongozi wa biashara yako.
Kila jambo linalokutokea kama mjasirimali au mtu wa kawaida ni matokeo ya uchaguzi wako wa awali. Angalia
mfano huu, tukio (event) unapata shilingi 250,000/, uamuzi wako (response)
unazitumia hizo hela kwenye vilabu maarufu unavyovifahamu kwa kuwafurahisha
watu wako(people behind you), matokeo ya uamuzi wako (outcome) unaishi maisha ya ‘tafadhali
nipigie’ na kuendelea kulaumu watu wasiopaswa kulaumiwa hasa serikali.
Mfano wa pili ni kinyume cha huo hapo juu. Tukio (event) unapata shilingi
250,000/, uamuzi wako (response) unawekeza
hizo hela kufungua mradi mdogo ama kwa kulipia semina za ujasiriamali, na kununua vitabu vya kujifunza ama kwa
kusomesha mtoto wako, matokeo ya uamuzi wako
(outcome) unakuwa umeandaa ndoto yako na hautaishi kwa kuisubiri
serikali au kiongozi wako.Unaondokana na vifafa vya kiuchumi. Unajua aina ya watu anaoshinda nao mtu
anapokuwa na fedha inaamua sana aina ya maamuzi anayoyafanya katika fedha
aliyoshika
Kwa kuhitimisha,
bado nitaendelea kutoa muda wangu kwa mtu atakae hitaji kuwekeza kwenye kilimo
cha miti, na mashamba ya kuuza bado yapo, nitakusaidia kama mimi nilivyo
saidiwa na watu wengine. “USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI
YA TANZANIA.
Sign up here with your email