.

Usijwekee Mipaka Kwenye Maisha

*Habari Za Leo Wanago-Big* Wenzangu? 

*Usijiwekee mipaka Kwa watu unaokutana nao Barabarani*  Ni Tafakari Yetu Ya Leo Kwa Ufupi. Kamwe Usikubali kukatishwa Tamaa Na Binadamu Yeyote kwenye Jambo unalolifanya.

Kuna siku Niliamua kwenda Soko la *Manzese lile la Nguo, When I want to know something I go for It* nimejijengea Tabia Ya Kutoka mkoa mmoja hadi Mwingine , ama kijiji kimoja kwenda kingine kujifunza mambo Ya Kilimo na Ufugaji, hasa baada Ya kugundua kwamba, Shule ama kusoma sina *Wito Kabisa* . Nilipofika pale kulikuwa na kelele za kila aina. Ukweli nilitaka kupata rafiki wa kuweza kunisaidia kukamilisha Somo langu.

Kwa mbele nikamuona kijana mmoja akiuza nguo za watoto, nikasogea Taratibu, nikamsalimia nikaanza kuchagua Nguo, Huyo Kaka Ana *strateji za Biashara Ya nguo ajabu*, kwanza Ana nyimbo za kumvutia mteja, Ana Piga Ngoma, na kuna Mdada pembeni Ana Piga vigelegele kweli Manzese ni zaidi Ya ujuavyo.

Niliaanza kumdadisi akaniambia Historia Yake Kwa Kifupi na alipo sasa kwakweli nikajifunza.

Mimi Nikaendelea kuchagua Nguo, nikanunua nguo zaidi Ya Mbili mara akaanza kuimba *Bro- Mwenye Tisheti Ya GoBig Mpende mwanao kabla hajawapanya rodi* Hahaha nikaongeza Nyingine Na Nyingine. (Biashara Ndogo ndogo ili utoke ndio kama hivyo) .

Kimsingi, kwenye Maisha,usjiwekeee mipaka, usiseme mimi Nitaishia Kumiliki Kitanda, ama simu, ama kumiliki rundo la marafiki wasiokuwa na *Tijakwako* , tunazo Nguvu tulizo umbwa nazo.

Kama ni MKULIMA kama Mimi, usiwaze kumiliki ekari Moja Tu, ama Mbili, hizo hazitoshi .

Wanasayansi wanasema kwamba, Kila kitu kina mvuto , wanaita *Atomu* ambazo zipo katika mzunguko ili kuweka mwendo wa Dunia katika mzunguko wake...

Kwakua sisi wanadamu tuna hisia, na hisia inaweza kuvuta kitu chochote, basi hakikisha hisia zako haziwavutii wavunja Malengo Yako. Hakikisha hisia zako zinawavutia watu Wenye Ndoto kama zako...Hao watu unaweza kuwapata Popote pale ulipo, Hata Hapa Gobig mbona matajiri Na WAJASIRIAMALI wakubwa sana wapo

Na Hii ndio Tafakari Yetu Ya Leo...
Ninawatakia Siku Njema Yenye Mafanikio makubwa sana.

*Wakomtiifu Meshack MAGANGA Mfuasi wa Mpango wa Elimu Kwa waliokimbia Umande Yaani MEKU lakini nikajielimisha sana kupitia kujifunza Kwa wakimbia umande wenzangu*

Latest
Previous
Next Post »