Na: Meshack Maganga---Go BIG
Maelezo kwa masaada wa Jarida la Mkulima Mbunifu
Bamia ni zao linalolimwa sana nchi za joto. Zao hili hutumika kama mboga inayoliwa matunda
Asili
ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili
limeenea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia
na Philipines. Zipo aina nyingi za bamia, aina zile za kiasili nazo
hutofautiana kulingana na eneo moja na lingine.
Matumizi
Bamia
hupikwa pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine. Aidha majani yake pia
huweza kuchumwa yakiwa bado machanga na kutumiwa kama mboga nyingine za
majani.
Lishe (SOMA ZAIDI)
Zao
la bamia lina virutubisho vingi ambavyo ni muhimu kwa miili yetu kama;
•
Madini ya chokaa ambayo hujenga meno na mifupa
•
Husaidia sehemu za viungo mbalimbali vya mwili kama sehemu za magoti, utumbo na
macho.
Udongo
Bamia
humea na kukua vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha na udongo
usiotuamisha maji. Aidha, kama ardhi haina rutuba ya kutosha, ni vyema kuweka
mbolea ya mboji au samadi.
Hali
ya hewa
Zao
hili hustawi katika mita 1,000 kutoka usawa wa bahari na haliwezi kuvumilia
hali ya baridi kali.
Uoteshaji
•
Shamba la bamia ni vizuri lilimwe mapema kabla ya kuotesha bamia.
Mbegu
•
Mbegu bora zenye kutoa mavuno mengi zichaguliwe.
•
Mbegu za bamia huota kwa shida, mara nyingi huchukua siku nane hadi 12
kutokeza. Ili kurahisisha uotaji, inapendekezwa kulowekwa mbegu kwa muda wa
siku moja kabla ya kuotesha ili kurahisisha uotaji.
•
Mbegu mbili zipandwe kwenye shimo moja.
Nafasi
Nafasi
ya upandaji iwe ni sentimita 30 toka shimo hadi shimo na sentimita 50 toka
mstari hadi mstari. Kwa zile aina zinazorefuka sana iwe sentimita 40 kati ya
shimo na shimo na sentimeta 70 kati ya mstari na mstari.
Bamia
inapotunzwa vizuri humpatia mkulima nafasi nzuri ya kujiongezea pato kwa kuwa
hupata bei nzuri sokoni tofauti na bamia ambayo haikutunzwa vizuri.
Hakikisha
shamba ni safi wakati wote kwa kuondoa magugu mara tu unapoona yamejitokeza.
Umwagiliaji
Iwapo
unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia
maji bustanini.
Wadudu
waharibifu
Wadudu
wanaoshambulia zao hili la bamia kama vile kimamba, funza wa vitumba na utitiri
mwekundu.
Magonjwa Na changamoto..
Kushuka kwa soko na kutokuwepo kwa soko la uhakika
Magonjwa
kama ukungu, ubwiri poda na kunyauka huathiri zao la bamia hivyo ni vyema
kuzuia kwa kufuata mzunguko wa mazao na kutumia dawa kulingana na ushauri wa
wataalamu wa kilimo.
Mambo
ya kuzingatia
•
Tumia mbegu bora
•
Panda kwa nafasi
•
Mwagilia maji ya kutosha
•
Palilia shamba vizuri
•
Vuna kwa wakati unaotakiwa
Uvunaji
•
Bamia huvunwa kabla ya kukomaa yaani zikiwa bado changa.
•
Kiasi cha kilo 8,000 zaweza kupatikana katika ekari moja iwapo zitatunzwa
vizuri.
•
Hakikisha unavuna bamia na kikonyo chake, kisu kinaweza kutumika kwa kuvuna.
Unaweza kujipatia hadi shilingi elfu 60,000/ kwa roba moja la Bamia
Meshack Maganga---Go Big Or Go Home
Sign up here with your email