.

Sababu Kumi Za Kubaki Kwenye Ajira Kabla Ya kwenda Kwenye Ujasiamali...!


  Na: Makirita Amani -- 
 
Kwanza nikupongeze sana kama wewe ni mmoja wa watu hawa ambao wanaona kazi pekee haitawawezesha kufikia yale mafanikio makubwa waliyopanga kufikia. Pamoja na ajira kutokuweza kukufikiahsa katika malengo yako makubwa, pamoja na changamoto nyingi zilizopo kwenye ajira, bado ni muhimu wewe kuendelea kuwepo kwenye ajira hiyo kwa muda kabla hujaiacha na kuingia moja kwa moja kwenye ujasiriamali. Hapa nitakupa sababu kumi kwa nini nakuambia hivi.

Kabla hatujaangalia sababu hizi kumi kwanza tuangalie upotoshwaji ambao umekuwa unafanywa kwa wengi. Watu wengi wamekuwa wakiaminishwa kwamba, kama unataka kuw amjasiriamali mwenye mafanikio, basi unahitaji kuchukua mazingira hatari (risk taker). Kama upo kwenye ajira basi uachane na ajira hiyo na kuingia kwenye ujasiriamali ambapo utaweka nguvu zako zote na kuweza kupata kipato kinachoendana na juhudi zako. 
Maelezo haya ni ya kweli ila hayamalizii kipande muhimu sana cha maelezo hayo ambacho ni biashara zinazoanzishwa na watu ambao hawana uzoefu wowote wa biashara, kati ya kumi, nane zinakufa ndani ya mwaka mmoja mpaka miwili. Na biashara zinazoanzishwa na watu ambao walishawahi kufanya tena biashara, sita kati ya kumi zinakufa kati ya mwaka mmoja mpaka miwili.

Kuingia kwneye biashara ambayo watu nane kati ya kumi watashindwa, ni hatari kubwa sana kwa mtu yeyote, kwa sababu hii ni sawa na kuwa na uhakika kwamba unakwenda kushindwa kwenye biashara hiyo.

Nimekuwa nikishauri watu wanaoingia kwenye biashara na ujasiriamali kwa muda sasa lakini sijawahi kumwambia mtu aache kazi haraka ili aweze kuweka nguvu zake kwenye ujasiriamali. Nina sababu nyingi kwa nini sifanyi hivyo, na hapa nitakushirikisha sababu kumi.

1. Unahitaji kuendelea kuwa na kipato cha uhakika. Japokuwa kazi haina uhakika sana kwa sasa, lakini angalau kwa sasa kuna kipato ambacho unakipata kwenye ajira yako. Hiki kitakuvusha nyakazi ambazo ni ngumu, hasa pale ambapo utaanza ujasiriamali ukiwa bado kwenye ajira yako.

2. Kuna nafasi nyingi za kuweza kuanza ujasiriamali hata bado ukiwa kwenye ajira yako. Tumia nafasi hizi na anza kidogo kidogo, jifunze kenye kila hatua unayoshindwa au kukosea, endelea kukuza biashara yako na ikifikia hatua ukaona sasa hapa inaweza kukupatia kipato cha kutosha kuendesha maisha yako ndio unaweza kuacha kazi.

3. Kutoa fedha kwenye biashara changa ni kuiua. Katika miezi angalau sita ya kwanza ya biashara yoyote ndio kipindi ambacho biashara yoyote inakazana kukua. Sasa kama utaondoa fedha kwenye biashara hii kwa sababu yoyote ile, unakuwa umeandika adhabu ya kifo kwneye biashara yako. Unahitaji kuendelea kuwa na kipato kingine unachotegemea tofauti na biashara hiyo, hivyo kama umeajiriwa, hiki ndio kipato chenyewe.

4. Kukuza mtandao wako wa kibiashara. Unapokuwa kwneye kazi ni rahisi sana kukuza mtandao wako wa kibiashara. Unaweza kutengeneza wateja wengi wa huduma au bidhaa zako kupitia kazi unayofanya hivyo inakupa nafasi nzuri ya kuweza kukuza biashara yako.

5. Kufaidi huduma nyingine muhimu. Kuna huduma muhimu ambazo utaweza kuzifaidi kama utakuwa kwenye kazi. Kupitia kazi yako unaweza kuwa unapata huduma ya bima ya afya kwako na kwa familia yako. Hii inakusaidia kuokoa fedha nyingi ambazo ungezitumia kwenye huduma za afya. Japokuwa unaweza kujiunga na mfuko wa bima ya afya kama mtu binafsi, bado itakugharimu kiasi kikubwa kuliko aliyeko kwneye ajira.

6. Kazi inaweza kukupa uzoefu wa biashara. Kuna baadhi ya biashara unazoweza kuanzisha ambazo zinaendana na kazi unayofanya sasa. Kwa kuwepo ndani ya kazi ile unajifunza mambo yote muhimu ya kuzingatia ili na wewe uweze kukuza biashara yako. Pia unawajua vizuri wateja ambao wanaweza kuja kuwa wateja wako pia na mambo mengine ya ndani ambayo yatakuwezesha kuendesha biashara yako vizuri.

Kuendelea kusoma sababu zilizobaki na hatua za kuchukua kama wewe ni mwajiriwa na hata kama sio mwajiriwa, jiunge na KISIMA, KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA nonyeza hayo maandishi, jaza fomu na tuma fedha ya ada ya uanachama. Kupata makala nzuri na pia kuingia kwenye group la wasap ambalo lina mijadala mbalimbali ya kukuwezesha kufikia mafanikio, lipia ada ya GOLD MEMBER ambayo ni tsh elfu 50 (50,000/=) kwa mwaka.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa.

TUPO PAMOJA
Makirita Amani
makirita@kisimachamaarifa.co.tz




Previous
Next Post »