.

Kuna Wakati Inabidi Ufe Ndani Kidogo

 Na: Mrope wa Mrope

Kumbe kuna wakati inakupasa kujitafakari, kujua ulipo na kuangalia unakoelekea kisha ujipime kama kweli utaweza kufika kwa namna ulivyo? Ukishajua wapi unakwenda na upenyo unaoendea upoje itakuwa rahisi kwako kujiweka sawa ili upite; yawezekana unapotaka kupita ni mlango mwembamba lakini wewe ni
mnene (majisifu, jeuri na kiburi) itakubidi upunguze unene (ujishushe, kujinyenyekeza na utii) ili uweze kupita. Kwa hiyo utagundua labda wewe ni mfupi (tuseme hujitumi) lakini unapotakiwa kupita inabidi uwe mrefu (ujitume) ili uweze kupita na mifano mingine mingi.
Jambo muhimu ni kuangalia unaweza kufika unakokwenda kwa namna ulivyo au unahitaji kubadilika? Mara nyingi nimekuwa nikisisitiza kuhusu kuhama.
Ili ufike unakokwenda lazima akili na mawazo yako  yahamie kule unakotaka kufika ili mwili uburuzwe kuelekea unakotaka kufika.
Jipime kwanza, kwa mwendo huo wa mawazo, matumizi, marafiki, mtazamo, unayosoma na unayotazama yanafanana na watu wanaoelekea huko unakoelekea? Utagundua unahitaji kufa (kubadili namna ulivyo/kulipia gharama ya mafanikio yako ikiwepo kubadili marafiki, mtazamo, unayosoma, magroup ya whatsup, marafiki wa fb na mengne mengi) kisha uzaliwe upya (kupokea badiliko kwa kuwa na kila kitu kipya kinachoendana na unakoelekea).
Nimependa kulinganisha kubadilika na kufa kwa kuwa badiliko la kuachana na mambo uliyozowea si jambo jepesi unatakiwa kujitoa kweli kweli lakini kama unajua nini unataka wala haitakuogopesha hata kama inauma.
Ili mgonjwa mahututi katika magonjwa mengi ili apone anatakiwa kufanya oparesheni wengne husema nusu kaputi ili apate kuwa mpya mwenye uzima na afya tele.
Oparesheni ni kufa na kupona na kwa namna hiyo mtu huyo anakufa kwa muda fulani ili awe mpya mwenye nguvu tele.  Ili kufika unakotaka jipime na uone kama kweli upo ktk safari ya kwenda unakokwenda au upo safari ya kurudi unakotoka? Utabadilika au utabaki ulivyo???
ALOYCE MROPE, Che Mrope Wa Mrope (fb), Mbeba Maono (fb page) 0766656626/0715366010



 
Previous
Next Post »