Na : Albert Sanga - Iringa
Kimsingi kwenye maisha kila mtu, kuanzia watoto mpaka watu wazima fedha
hupita mikononi mwao; kinachotofautiana ni viwango. Kwa hiyo, utaona
kuwa kupata fedha sio tatizo kwa sababu wengi(kama sio wote) tumewahi
ama huwa tunapata fedha. Kazi mbili ngumu linapokuja suala la
fedha ni
kutunza na kuziongeza fedha zinazopita kwako ama unazopata.
Hapa ndipo
"tunapoachana na kupotezana" kiuchumi. Hekima inatuambia kwamba fedha
yeyote inayopita kwako, (iwe ya kupewa, uwe mshahara, iwe faida, iwe
mkopo ama vyovyote) ni lazima uichukulie kama mbegu; kwanza izalishe
thamani ndipo itoke, kinyume na hapo fedha haiwezi kuvutiwa kuishi na
wewe. ~SmartMind~
Sign up here with your email