.

You Don't necessarily Have To think Big as Google or You Tube...


                      Mashine ya kisasa wood mizer ya Rich Dad wangu
 Nilipewa nafasi ya kuongea na wageni walioenda kumtembelea Rich Dad wangu

 Meshack Maganga--Iringa.

You don't necessarily have to think Big as Google or You Tube... Think about what actvities or things you absolutely love to do and get you exited regardless of the money. Imekuwa siku ya
mafanikio makubwa kwangu. 

Nilipigiwa simu juzi na Rich Dad wangu (Mzee ninaempenda sana hapa duniani). Aliniita nikajifunze uandaaji wa miche ( kwa sababu tuna miezi minne tu kabla ya kuanza kupanda miti ya 2016) Ni pamoja na kiwanda chake alichokifungua kinachotumia machine za kisasa kama hii ya "WOOD-Mizer" ni machine inayokuwezesha kutengeneza mbao na magogo kwa mtindo unaoutaka wewe. 

Na makapi yanayobakia yaani ule uchafu wa mbao ama pumba ya mbao inatengenezwa mbolea, nyingine inatumika kutengenezea fenicha za kisasa. Nimetembelea mabanda ya Mifugo kama Ng'ombe, kuku, bata mzinga, kanga, mbuzi. Kilimo cha parachichi, Nguzo, Nk. Nimeingia ofisini kwake, amenimbia kwakuwa mwaka unakaribia kumalizika inabidi nijipange kwa kutumia muda vizuri. Maana muda una thamani kuliko pesa. Akaniasa kutafuta maaana katika maisha. 

Kweli nimejifunza na ninaelekea porini kuanza upya kabisa upandaji miti, maana kwenye uwekezaji wa kilimo cha miti kuna mapya kabisa, kuna mbegu mpya, uchimbaji wa mashimo ya kuweka miti kwa mtindo mpya nk.

 Mission and plan are only the beginning. You don't necessarily have to think big as Microsoft or Google or You Tube. Take baby's step, let your passion pull you forward. But the choice is up to you nobody else. Go Big Or Go Home.


























Meshack Maganga---Go Big Or Go Home
Previous
Next Post »