Unaweza kujiajiri kupitia kilimo cha vitunguu..!
Ndugu
zangu, wiki iliyopita nilihamsika sana baada ya baadhi ya wasomaji kuniandikia
barua pepe na wengine kunipigia simu kutaka ufafanuzi kuhusu kilimo cha Maembe,na
kilimo cha miti na organic farming kwa ujumla, kilimo ambacho nilianza nacho
miaka mitatu iliyopita nikitokea shuleni.
Mwaka uliopita niliandika makala
kuhusu wasomi kujifunza kujiajiri nilikusudia kuwasilisha ujumbe mmoja
ya kwamba, “Wasomi na watanzania kwa ujumla wetu tunatakiwa kubadilisha mitazamo yetu ili kujipatia mipenyo ya
kiuchumi na kifedha (financial freedom.
Kimsingi ni kwamba zipo
imani zinazosapoti watu kuwa na fedha za kutosha na zipo imani na mitazamo inayozuia watu kuwa na fedha ama inawafanya waishi maisha ya kupungukiwa nyakati zote! Imani na mitazamo hii kimsingi huzalishwa kutokana na malezi, utamaduni na mazingira. Mtazamo wa mtu kuhusu fedha tunaita, “Money blue print” .
imani zinazosapoti watu kuwa na fedha za kutosha na zipo imani na mitazamo inayozuia watu kuwa na fedha ama inawafanya waishi maisha ya kupungukiwa nyakati zote! Imani na mitazamo hii kimsingi huzalishwa kutokana na malezi, utamaduni na mazingira. Mtazamo wa mtu kuhusu fedha tunaita, “Money blue print” .
Nafahamu kuwa wengi kama sio wote tunakubaliana
kuwa fedha zina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya mtu, na kwamba ukosefu wa
fedha ndio msingi wa maovu(Ingawa wapo watu wanatumia fedha kufanya uovu wao)
tunachotofautiana ni imani kuhusu fedha. Mitazamo kuhusu fedha ndio inayoamua
kiwango cha fedha alichonacho kila mmoja. Hii ina maana kuwa kila mtu anamiliki
kiwango cha pesa sawa sawa na imani ama mtazamo wake kuhusu fedha.
Miaka michache iliyopita wakulima walikuwa ni
watu wanaotazamwa kama watu wenye shida, walio jitokeza kuwekeza kwenye kilimo
walionekana wameshindwa shule ( waliokimbia umande). Na hii ilisababishwa na
imani ama mapokeo ya tuliyorishwa na wazazi wetu na walimu wetu kutoka kwenye
kipindi cha zama za viwanda (Industria Age). Lakini kwa sasa dunia imebadilika
sana, kilimo kimewafikisha watu kwenye ndoto zao, Nimesoma kwenye jarida la Forbes kwamba tajiri wa
kwanza Afrika amewekeza kwenye kilimo, wajarisiamali wakubwa hapa Tanzania
wamewekeza kwenye kilimo, na wale wanaojiona wameenda shule ‘middle class’
wanaendelea kushangaa na kuendelea kuongea sentensi hasi na kulalamikia viwango
vidogo vya mishahara.(Kazi kweli kweli).
Miaka ya
hivi karibuni kwenye Mikoa ya Arusha, Manyara, Iringa,
Mbeya,Tanga, Singida na Kilimanjaro zao
la vitunguu limejizolea umaarufu mkubwa kwa kuendelea kuajiri maelfu ya
Watanzania. Kuna ambao wamefikia ndoto zao kupitia kilomo cha vitunguu,
wamejenga nyumba, wamefungua makampuni yao, wanasomesha watoto nk. Vitunguu
hivi hivi kuna rafiki zangu wamenunua magari ya ndoto zao, wamejipa likizo nchi
za nje.
Nitaongelea hasa eneo la Mahenge
sehemu ninayolima mimi. Hali ya hewa na maji ni vipengele muhimu sana vya
kuzingatia katika uzalishaji wa zao la vitunguu.Vitunguu vinastawi vizuri
katika hali ya ukavu kwa kutumia umwagiliaji.(Local Irrigation) Maji mengi hasa wakati wa masika husababisha
magonjwa mengi hasa ukungu, vitunguu haviwezi kukomaa vizuri, hivyo kusababisha
upotevu mkubwa wa mazao.
Aina ya mbegu tunayolima sisi pale Mahenge ni pamoja na
Mang’ola (traditional) red, Red creole na Bombay Red. Hizi ni mbegu bora ambazo
zinatoa mazao mengi kuanzia magunia 70- 90 kwa hekta ikiwa kilimo bora kitazingatiwa
na iwapo mkulima atakuwa anaongozwa na malengo yake na hamasa ya ndani (self
drive) Mkulima anaweza kuchagua mbegu kwa kuzingatia, soko, msimu wa kupanda
nk.
Wasambazaji wa mbegu ni pamoja na maduka
ya TFA, na maduka ya bembejeo za kilimo katika maduka mbalimbali. Ingawa wapo
baadhi ya watu hasa maeneo ya Ilula –Iringa ambao huandaa wenyewe mbegu kwa
kutumia maua ya vingunguu.
Uandaaji wa kitalu hutegemea sehemu husika, lakini kwa
kifupi Sehemu
ya kitalu iwe wazi, mbali na kivuli na kiwe karibu na chanzo cha maji na
huchukua takribani wiki tano mpaka sita kabla ya kupelekwa kwenye shamba
husika. Zipo changamoto mbalimbali ambazo hujitokeza kwenye maandalizi ya
kitalu mpaka shambani, changamoto hizo ni pamoja na wadudu, ugonjwa wa ukungu, Wadudu waharibifu
ni pamoja na Chawa wekundu ambao
wanashambulia majani, na wadudu waitwao Sota ambao hukata miche. Ili kudhibiti
tatizo, shamba likaguliwe mara kwa mara kuona dalili za mashambulizi. Endapo
kuna dalili za mashambulizi, mkulima –
mjasirimali ana shauriwa kuchukua hatua za kuzuia kabla uharibifu mkubwa
haujatokea ambao husabaisha wakulima wapya kukata tama na kurudi kule kule
kwenye kuilamikia serikali kwamba haiwajali.
Baada ya maandalizi ya kitalu na mbengu kupelekwa shambani,
hatua inayofatia ni ufatiliaji wa malakwamala kwa kupulizia dawa na palizi.
Iwapo mkulima yupo mbali na eneo husika, kwa mfano yupo Mwanza, Dar, Moshi ama
popote Duniani, mkulima atalazimika kuajiri vijana ambao watamfanyia kazi kwa
malipo mpaka vitunguu vitakapo komaa. Miche ya vitunguu, huota taratibu sana,
hivyo miezi ya mwanzoni, miche husongwa sana na magugu. Palizi mbili mpaka tatu
zinashauriwa na zinatosha kuweka shamba safi.
Kabla ya kuanza kuvuna vitunguu mkulima anashauriwa kukagua shamba ili kuhakikisha kuwa vitunguu
vimekomaa. Na iwapo upo mbali na shamba lako hakikisha unatembelea shamba lako
malakwamala. Dalili ya
vitunguu kukomaa ni, majani kunyauka na kuanza kukauka asilimia 80 -100% na
majani kukauka. Mpaka sasa hapa Tanzania, vitunguu huvunwa kwa mikono. Mimea
inangolewa au kuchimbuliwa kwa kutumia jembe dogo.
Baada ya kuvuna vitunguu vinaweza kuachwa shambani vikiwa
vimefunikwa na majani kukinga jua kwa
muda wa siku mbili au tatu kutegemeana na hali ya hewa. Lengo nikuimarisha ngozi(Nyama)
ya vitunguu nk. Pia kupunguza unyevu kwenye majani na mashina na kuruhusu sehemu
ya chini ya shingo kufunga. Ikiwa usalama ni mdogo, vitunguu vinachambuliwa na kukatwa
majani na mizizi na kuanikwa sehemu nyingine. Ukaushaji hutumia wiki mbili
kutegemea hali ya eneo.
Kwa sasa soko la vitunguu lipo juu
sana,Watu wa kada mabalimabali wanahusika na ununuzi na uuzaji wa vitunguu
wakiwa ni pamoja na: wakulima, wachuuzi, wafanya biashara ndogondogo, wauza
jumla, wauza rejareja, wasafirishaji na madalali. Kutoka shambani mpaka sokoni.
Kama nilivyotangulia kusema hapo
juu, hekari moja inaweza kutoa magunia 80-100 kwa sasa maeneo ya Njombe,
Iringa, na Kwingineko gunia moja la vitunguu huuzwa kati ya shilingi 130,000/= mpaka laki 150,000/= lakini mkoani
Njombe kwa bei ya sasa gunia moja ni shilingi 200,000/= kwa gunia. Ingawa kuna
baadhi ya misimu soko hushuka sana mpaka kufikia shilingi laki moja kwa gunia
ama elfu 70.(Kumbuka kwamba kutafuta pesa ni sawa na mchezo wa mpira wa miguu
kadiri unavyo ucheza ndiyo unavyo kuwa hodari-uchaguzi ni wako) Ukiwa na gunia
labda 70 ukaziuza unaweza pata hadi shilingi milioni milioni 9, kwa ekari moja
baada ya kuondoa gharama yote. Sasa ukiwa na ekari 5, 6,ama 3 utakuwa na
shilingi ngapi? Wakati huo unasubiri mshahara wako. Kaka yangu mimi kwa msimu
uliopita alipata magunia 1000, ni utajiri gani huu?
Kila mtu anayo nafasi sawa (equal
channce) ya kuwa na fedha za kutosha kumpa uhuru wa kiuchumi. Pili hakuna raha
wala sifa ya kuendelea kuwa masikini, kama unafikiri nisifa ama unajidanganya kuwa masikini
watapunguziwa adhabu siku ya mwisho unapoteza muda wako kwa sababu masikini ni mzigo kwa dunia.
Masikini na umasikini wake hata awe ni mtakatifu na mwema kiasi gani ni kwamba
anaitesa dunia (kwa sababu anahitaji kusaidiwa). Tajiri (ama niseme mwenye
fedha za kutosha) hata kama ni mchoyo ama bahiri bado ni msaada kwa dunia (kwa
sababu anajisaidia).
Ninatamani kila mmoja apokee changamoto ya kutamani kuwa na uhuru wa kifedha na
kiuchumi kwa kuanza na vitu
tunavyo viona ni vidogo kwenye macho yetu ama kuachana na kasumba tuliyopewa
shuleni kwamba ukimaliza kusoma lazima usake ajira. Ajira zenyewe hakuna na zilizopo bado ni chache. Na hili linawezekana
ikiwa mitazamo na imani za wengi kuhusu fedha zitabadilika na kuwa zinazosapoti
badala ya kuvuruga nafasi ya mtu kupata fedha.Kila mtanzania anastahili ushindi wa kifedha. Wengi wetu tumekuwa watu wa kuhangaikia malengo ya
wenzetu, kuna watanzania wenzetu wapo tayari kuzungumzia Malengo za timu za
ulaya siku nzima, wiki, mwezi na jinsi
ya kuhakikisha wanapata ushindi nk, mtu huyohuyo hana ajira, ama ajira aliyonayo
mshahara hautoshi.
Kwa watanzania watakao penda kufanya kilimo hiki ama kile cha miti wanaweza
kunitafuta nikawapa maelezo ya kutosha.Nchi hii ina matatizo mawili ya msingi
kwenye kipengele cha Ujasiriamali, kuna wanaozifahamu fursa lakini hataki
kuziweka wazi, sijuwi wanaogopa nini?
Labda wana hofu ama ni wachoyo.Na kuna wale ambao walishazisikia fursa
lakini bado wanasema nitaanza kesho na kuna wale wanaosingizia mitaji, umbali
nk.
Meshack Maganga 2014
Sign up here with your email