Na: Meshack Maganga, Go Big Iringa...(Picha na maelezo kwa Hisani ya Mkulima mbunifu... )
Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.
Papai ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.
Uzalishaji wa papai nchini Tanzania
ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji ya watumiaji, hivyo inahitajika
nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao hili.
UHUSU MPAPAI
i) Mpapai wenye maua kiume tu ii)
Mpapai wenye maua kike tu iii) Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite
papaya)
Katika uzalishaji kila aina ya
mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa
mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote
hauhitaji mpapai wenye maua ya kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.
Kutokana na jinsia ya maua mpapai
huweza kutengeneza matunda yenye maumbo tofauti. Matunda yanayotengenezwa
kutoka katika mpapai wenye maua ya kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au
yenye umbo la yai na matunda yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote
mbili huwa na umbo la refu zaidi au umbo la pear.
UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI
Miche ya mpapai
Katika uzalishaji wa miche ya mpapai
kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika: -
1. Mbegu za Kawaida (Local seeds)
Hizi ni mbegu ambazo huweza
kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina hii ya mbegu ni vigumu kujua
kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye jinsia zote. Hivyo itakulazimu
kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua hivyo kuacha majike na
yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50
ya mipapai yenye maua ya kike.
2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)
Aina hii ya mbegu ni nzuri kwa
sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamaoja
(Hermaphrodite papaya)na pia hukua haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao
mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1, MALAIKA F1 n.k.
Upandaji
Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba
chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha weka viriba
vyako venye mbegu chini ya kivuri kisha mwagilia maji. Baada ya kumwagilia
unaweza pulizia kiasi kidogo cha kiuwatilifu (fungicide & Insecticide)
kwenye udongo wako ili kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea wako.
Mbegu ya papai uweza chukua
siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo. Hivyo hakikisha unamwagilia maji
kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa toka
kwenye kitalu baada ya wiki sita hadi nane.
Kitalu cha mipapai
BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA
ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI
Mpapai upendelea zaidi udongo
unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na wenye makadilio ya Ph 6.5.
Inapowezekana zuia kupanda mimea
yako kwenye udongo wa mfinyanzi na wenye magadi.
Kiaisi cha maji kilichopo kwenye
udongo huweza kuonyesha ukubwa wa matunda. Eneo lenye udongo wenye unyevunyevu
mwingi huweza tengeneza matunda makubwa na yalioja maji maji na eneo lenye unyevunyeku
kidogo hutengeneza matunda madogo na magumu.
Mpapai hawezi kuvumilia upepo mkali,
maji yaliotwama pamoja na ukame.
UANDAAJI WA SHAMBA
Njia ya kuandaa shamba
itategemea na eneo (topography), aina ya udongo, vifaa vinavyotumika kuhudumia
shamba.
Nafasi
Nafasi kati ya mmea na mmea ni mita
2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.
Andaa mashimo yenye upana na urefu
wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na wa juu. Kisha changanya udongo wa juu
na mbolea ya samadi. Katika kurushisha kwenye shimo tanguliza udongo
ulochanganywa na mbolea ya samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa chini
wakati wa kuchimba shimo.
NB: Kiasi
cha mmea huwa kati ya 1000 hadi 2000 kwa hekari ( 400 hadi 800 kwa ekari)
Kupanda mimea shambani
Baada ya hizo wiki sita hadi
nane hamishia mimea yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa mimea ufanyika wakati
wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa
mimea.
shamba la mipapai
Uwekaji wa mbolea.
Zuia matumizi ya mbolea zenye
chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine. Wiki moja baada ya kuhamisha
miche yako weka mbole gramu 28 kwa kila mche. Tumia mbolea yenye phospate kwa
kaisi kikubwa. Mfano; - 12:24:12. (NPK)
Baada ya hapo kila baada ya
wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa
mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK)
Potassium inahitajika kwa maua na
kuweka matunda hivyo tumia mbolea yenye potassium kiasi kikubwa mara baada ya
kuona mmea wako umeanza kuweka maua, kiasi cha gramu 114 cha mbolea
huitajika, fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2
(NPK) . Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron
kila mweze. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri.
Umwagiliaji
Maji ni sehemu ya muhimu sana katika
maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji niya muhimu sana katika kuweka maua,
matunda na ukuaji wa matunda. Katika ukuaji wa matunda hakikisha unaweka lita
23 kwa kila mmea kwa wiki.
Magugu
Hakikisha unazuia magugu kipindi cha
mwanzo ili kuzuia ushindani kati ya mimea na magugu kwa virutubisho na maji. Na
pia kuzuia magugu kubeba vimelea na wadudu wanaoweza kuathili mazao yako.
HATUA ZA UKUAJI WA MPAPAI
Kitalu - Wiki 1 - 6
Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya
kuamishiwa shamba - wiki 7 -16
Maua na kuweka matunda - wiki 17 -
21
Kukua kwa matunda - 22 - 26
Mavuno ya kwanza - Wiki 37
nakuendelea .................
a
Meshack Maganga---Go Big Or Go Home
Sign up here with your email